Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan
........................................
Kuna simulizi ambazo haziandikwi kwa wino pekee, bali huchorwa kwenye mioyo ya watu kwa machozi, furaha na mshangao wa kweli. Kagera leo imeshuhudia historia hiyo—historia inayotufundisha kuwa kuna viongozi wanaoweza kuwa madaraka yao ni heshima ya kuwahudumia watu, si majivuno ya vyeo. Na jina linabaki moja tu: Samia Suluhu Hassan.
Katika jiji dogo la Bukoba lililopo mkoani Kagera, lenye kumbukumbu chungu ya mafuriko ya Mei 10, 2024, bado makovu ya maji yanayoangamiza makazi hayajafutika. Lakini katikati ya makovu hayo, imechipua tumaini jipya. Ni tumaini lililojengwa kwenye msingi wa maelekezo ya Rais Samia, tumaini lililofungwa kwa tofali na saruji, na leo likasimama kama kioo cha upendo wa kweli.
Ni nyumba. Lakini si nyumba tu. Ni kimbilio, ni hadithi, ni muujiza. Nyumba ya vyumba vitatu iliyokabidhiwa rasmi kwa Bibi Catherine Nathahiel—mama wa taifa hili kwa namna yake mwenyewe, anayelea wajukuu sita waliopoteza wazazi....SOMA ZAIDI
0 Comments