Jina langu ni Brian Otieno, mwenyeji wa Kisumu. Kuna kipindi nilihisi maisha yamenipita. Nilikuwa nalala kwa rafiki yangu baada ya kushindwa kulipa kodi ya nyumba yangu ndogo. Nilitembea jua kali nikitafuta kazi, lakini kila mlango niliobisha ulikuwa unaonekana kufungwa. Wakati marafiki zangu walikuwa wanaendelea kimaisha, mimi nilihisi kama dunia imenigeuka. Nilikuwa nimeanza kukata tamaa kabisa.
Siku moja niliketi kando ya barabara nikijiuliza nitakula nini siku hiyo. Nilikuwa nimebeba bahasha yenye vyeti vyangu vya elimu, lakini havikusaidia chochote. Nilihisi aibu hata kuongea na familia yangu. Nilijiona kama mtu aliyeshindwa na maisha. Nilikuwa na ndoto ya kuanzisha biashara yangu, lakini nilikuwa sina hata mia moja mfukoni.
0 Comments