SIMBA SC YATAMBULISHA KOCHA MPYA KUWANOA CAMARA, YAKOUB

Subscribe Us

SIMBA SC YATAMBULISHA KOCHA MPYA KUWANOA CAMARA, YAKOUB

 Simba SC imemtambulisha kocha mpya ambaye atakuwa anawanoa makipa watimu hiyo kwa msimu wa 2025/26 kwenye mechi za ushindani.

Anaitwa Vitomir Vutov ametambulishwa rasmi kuwa kocha wa timu hiyo yenye maskani yake Kariakoo mtaa wa Msimbazi.

Ni Hussen Abel, Moussa Camara na Yakoub Suleiman haw ani makipa wa Simba SC watanolewa na mwalimu huyu mpya ambaye ametambulishwa rasmi Oktoba 15 2025.

 Vutov ana umri wa miaka 53 aliwahi kuwa kocha wa makipa katika klabu mbalimbali ikiwa ni Litex Lovech, Bulgaria U17, Bulgaria U 19.

Kwa sasa kikosi cha Simba SC kipo kwenye maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wao ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nsingizini ya Eswatini unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 19,2025 na leo Oktoba 16 2025 msafara unatarajiwa kuondoka kuelekea Eswatini.SOMA ZAIDI

Post a Comment

0 Comments