BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI NI HATUA MPYA, KASI MPYA, NA MUSTAKABALI MPYA" - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Monday, 17 November 2025

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI NI HATUA MPYA, KASI MPYA, NA MUSTAKABALI MPYA"


Na Godwin Myovela, Dodoma
.....................................

Katika hatua  iliyoonyesha ukomavu wa kisiasa, uthubutu wa kiuongozi na dira mpya ya maendeleo, Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza Baraza jipya la Mawaziri — mabadiliko ambayo kwa mara nyingine yanaweka wazi namna taifa linavyoingia katika hatua mpya ya uwajibikaji, utendaji na uwiano wa kimkakati.

Pia amewaacha nje baadhi ya mawaziri maarufu na waliozoeleka miongoni mwa watanzania jambo linalotafsiriwa kama ujumbe mzito kwa taifa na kwa wanasiasa kwamba mageuzi si adhabu, bali ni sehemu ya safari ya kujenga utawala unaotanguliza matokeo.

Kwa kuachwa nje mawaziri kama Dk. Doto Biteko, Hussein Bashe, Innocent Bashungwa, Jenista Mhagama, Dk. Seleman Jafo, Dk. Pindi Chana na Dk. Damas Ndumbaro, Rais Samia ameonyesha ujasiri wa kisiasa unaozingatia tathmini ya matokeo, usawa wa uwezo, na mzunguko wa mawazo mapya serikalini.

Ingawa wote hawa wanaendelea kubaki na nafasi zao za ubunge, hatua ya kutowapa tena dhamana za uwaziri inatoa picha mbili muhimu; kwanza serikali inataka kasi mpya ya utekelezaji, na pili uongozi — ni jukumu lenye mizani ya utendaji.

Katika kipindi ambacho taifa linajikita kwenye mageuzi ya kiuchumi, diplomasia ya kimkakati, usimamizi wa rasilimali, na ujenzi wa mifumo imara, hatua hizi zinatafsiriwa kama sehemu ya “recalibration” yaani  kusawazisha upya msukumo wa maendeleo.

Rais Samia amekuwa akisisitiza juu ya suala la efficiency, accountability na results-oriented leadership.

Hivyo, kutangaza Baraza jipya ni kuanzisha hatua mpya katika kuongeza ufanisi wa serikali katika sekta zinazobeba uzito wa uchumi (nishati, kilimo, viwanda, sheria na uwekezaji).

Azma hasa ni kuhakikisha kasi ya mageuzi inakwenda sambamba na matarajio ya wananchi, ndio sababu hasa amejikita kuweka uwiano wa kizazi kipya na uzoefu, huku akiruhusu damu mpya yenye ubunifu kuingia kwenye mfumo.

Mabadiliko haya ni ishara kwamba Tanzania inaingia kwenye hatua ya pili ya ajenda ya mageuzi chini ya utawala wake — hatua ya utekelezaji wa kina, uthabiti wa uchumi, na ushirikishwaji mpana wa wananchi.

Kwa wanasiasa, hii ni ishara ya kutafakari. Si kila anayeondolewa kwenye nafasi anakosolewa; wengine wanapisha mwelekeo mpya, mikakati mipya, au mizani ya usawa wa kitaifa.

Kwa taifa, ujumbe ni mmoja; Tanzania inaelekea kwenye hatua ya uongozi unaoishi kwa matokeo, si kwa miiko ya kisiasa.

Baraza hili litategemewa kusukuma mbele mageuzi ya sekta ya nishati, ikiwa ni pamoja na kuharakisha uwekezaji na upatikanaji wa umeme wa uhauhakika

Pia, kuinua kilimo cha kisasa, thamani ya mazao, na ujenzi wa mfumo shindani wa chakula, sanjari na kuimarisha mifumo ya afya, sheria, utalii na biashara, kwa msukumo mpya na matokeo yanayopimika.

Aidha, kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha wananchi moja kwa moja, kwa uwazi, uwajibikaji na ufanisi.

Mabadiliko haya yanaonekana kama sehemu ya mkakati mpana wa Rais Samia wa kujenga Tanzania yenye uchumi thabiti, taasisi hai, na serikali inayofanya maamuzi kwa maslahi ya wananchi.

Hatua kama hii ndizo zinazoandika sura mpya za mwelekeo wa taifa. Tanzania ya sasa inatazama mbele — taifa linalojifunza, kujirekebisha na kusonga kwa kasi ya ushindani wa kanda na dunia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad