Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu CPA Francis Kafuku akizungumza katika tukio la ugawaji wa miche hiyo amewataka wananchi kuchangamkia kilimo cha zao hilo na kueleza kuwa ni fursa kwao hasa ya kukabidhiwa miche hiyo pasipo gharama yoyote.
Aidha, CPA Kafuku alisema wilaya hiyo kujikita katika kilimo cha zao hilo la biashara ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akihimiza ubunifu wa kilimo na masuala mengine ili kuwakomboa kiuchumi wananchi na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake, Diwani Mteule wa Kata ya Buhoro, Charles Kinele, alisema licha ya wananchi wengi wa eneo hilo kujikita zaidi katika kilimo cha chakula wanakila sababu ya kujielekeza katika kilimo cha biashara ambacho kitawainua kiuchumi.
Awali, Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri hiyo, Mikidadi Mbaruku alisema kuwa uzalishaji wa miche hiyo unafanyika kwa ushirikiano na Bodi ya Kahawa Tanzania kwa kushirikiana na Halmashauri ambayo hutenga eneo kwa ajili ya vitalu vya miche.
Mbaruku alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi kwa kushiriki kikamilifu kuitunza miche hiyo hadi kufikia hatua ya kupelekwa shambani.
Mkulima Noadia Konge akizungumza kwa niaba ya wenzake kutoka Kijiji cha Her Ushingo alisema atawahamasisha wenzake, hususan wanawake, kujiunga kwenye kilimo cha zao hilo chenye tija.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Francis Kafuku akizungumza wakati wa ugawaji wa miche hiyo Novemba 18, 2025.








No comments:
Post a Comment