Mmoja wa mwananchi akipata maelezo alipotembelea mabanda katika maonesho ya mashine mbalimbali za kilimo, ufugaji na ujenzi zinazozalishwa na kusambazwa nchini na Kampuni ya Poly Machinery yaliyo andaliwa na kampuni ya Poly Machinery yanayoendelea Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
.....................................
Na Godwin Myovela, Dodoma
Katika jitihada za kutimiza maono ya Dira ya Taifa 2550,
kampuni ya Poly
Machinery imedhihirisha kuwa teknolojia ya kisasa inaweza
kuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi, hususan vijana na wanawake.
Ofisi za kampuni hiyo zilizopo Dodoma zimekuwa kitovu cha
ubunifu na mafunzo yanayolenga kuongeza tija katika sekta za kilimo, ufugaji,
na ujenzi.
Baraka Mitimingi, Afisa Masoko wa Poly Machinery, amesema kila kukicha wanajitahidi
kusaidia jamii kwa kubuni na kuzalisha teknolojia zilizo rahisi kwa matumizi na
mtambuka kwa matokeo chanya, ustawi wa uchumi wa mtu mmoja na taifa kwa
ujumla.
Akizungumza jana ndani ya viwanja vya Nyerere Square kwenye
maonesho ya Wakandarasi na Wasambazaji wa vifaa vya Ujenzi nchini, chini ya
uratibu wa Mat Builders and Contractors Global Expo 2025 yanayoendelea,
alihimiza watanzania kutembelea banda lao na kuona mashine na teknolojia
mbalimbali zinazovutia.
Alisema kwa sasa wamebobea na kujikita kwenye uzalishaji na
usambazaji wa mashine za kupiga na kusafisha karanga, mashine za kupukuchua na
kusaga mahindi, pamoja na mashine za kukamua maziwa, alizeti na nafaka
nyingine.
Aidha, kampuni imewasilisha mashine za ufugaji za kisasa,
ikiwemo kunyonyoa kuku kwa mashine, kukata majani ya mifugo, na teknolojia za
ufugaji nyuki na ulinaji asali kwa tija, hatua ambayo inarahisisha kazi ngumu
kwa wanawake na kuongeza uzalishaji kwa wajasiriamali wadogo.
Maonesho haya pia yameonesha mashine za kuchanganya mchanga na
saruji, kuchanganya zege, na mashine za ufungaji wa tofali, ambazo ni nyenzo
muhimu kwa sekta ya ujenzi, na hivyo kutoa fursa ya kuongeza ajira na maendeleo
ya jamii.
Kwa mujibu wa Mitimingi, teknolojia hizi si tu zinarahisisha
kazi, bali pia zinatoa fursa
kwa vijana kuingia katika uzalishaji wa thamani kubwa na
kuanza biashara ndogo ndogo zenye faida endelevu.
Kwa wanawake, teknolojia hizi zinatoa nafasi ya kuingia katika
sekta za kilimo na ufugaji kwa kutumia mashine zinazopunguza kazi ngumu na
kuongeza tija, hatua muhimu katika uwezeshaji wa kijamii na kiuchumi.
Wataalamu wa Poly Machinery wamehimiza serikali na taasisi za
umma kuhakikisha teknolojia hizi zinatumika kikamilifu, huku wakiunga mkono
uwepo wa mafunzo ya kiufundi na urahisi wa kupata mashine kwa wingi.
Kampuni hiyo ina imani kwamba ushirikiano kati ya sekta binafsi
na serikali ni muhimu katika kufanikisha maono ya taifa, huku ikiwataka vijana na
wanawake kushirikiana na wajasiriamali wengine kutumia fursa hizi kuongeza tija
na kipato.
Maonesho hayo pia yamekuwa jukwaa la kushirikiana, kujifunza, na
kuona kwa vitendo jinsi teknolojia ya Poly Machinery inavyoweza kubadilisha
maisha ya wananchi na kuimarisha uchumi wa taifa.
Hata hivyo, baadhi ya wadau waliotembelea banda hilo wametahadharisha kwamba teknolojia kama hizi zinapotekelezwa kikamilifu, zinachangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha Dira ya Taifa 2550, kuongeza ushindani wa sekta za kilimo na ujenzi, na kutoa fursa ya biashara kwa vijana, wanawake na jamii nzima
Washiriki wa maonesho hayo hayo wakitoa maelezo kwa Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyererem Peter Mavunde ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyetembea mabanda hayo
Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyererem Peter Mavunde akioneshwa bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo.
Maelezo yakitolewa na washiriki wa maonesho hayo.











No comments:
Post a Comment