...................................
Na Dotto Mwaibale, Dodoma.
SHEREHE ya Kipaimara cha watoto Catherine Skana na Benjamin
Manase wa Chang'ombe Mtaa wa Mazengo Jijini Dodoma imekuwa ya aina yake kutokana
na sehemu kubwa kujaa nasaha na kufundwa huku wakielezwa kuwa nasaha hizo zitawasaidia katika maisha yao.
Sherehe hiyo ilifanyika baada ya ibada ya sakramenti ya ubatizo na kipaimara iliyofanyika Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kaskazini Usharika wa Nkuhungu Jijini Dodoma ambayo iliongozwa na Mchungaji wa Usharika huo Ephraim Mbise na muhubiri wa neno la Mungu alikuwa ni Mchungaji Ester Mwasyoge ambaye ni Mwenyekiti wa wilaya wa kanisa hilo katika jimbo hilo Dodoma.
Salome Daniel ni mama mlezi wa watoto hao ambaye alitumia
nafasi hiyo kuwasihi kuendelea kukua katika maadili mema kama ambavyo
wamekuwa wakielekezwa wakati wote.
“Babu na Bibi yenu Mzee Hebron Mwaibale ambao wametangulia mbele
ya haki tuliishi nao vizuri na walikuwa wakiwalea wazazi wenu katika misingi
mizuri ya upendo, kumuheshimu kila mtu na ndiyo maana na sisi tumeendelea kuwa nanyi na tuna wasisitiza mufuate nyayo zao,” alisema Daniel.
Daniel alisema wamehudhuria sherehe hiyo kutokana na
ushirikiano mzuri uliojengwa na babu na bibi yao ambao walikuwa ni rafiki wa kila mmoja
katika mtaa huo wa Mazengo.
Mama Amina ambaye ni jirani wa watoto hao aliwaomba watoto
hao waendelee kushikamana kama walivyo wazazi wao na kuwa hiyo ndiyo silaha
pekee ya kujilinda na mtu yeyote watakao muona anataka kuwatenganisha.
“Endelea kushirikiana na watoto wenzetu wa mtaa huu katika
masomo, kuwasaidia wazazi wenu kufanya kazi mbalimbali na kumheshimu kila mtu,
pasipo kusahau kusali jambo litakalowasaidia kufika mbali kimaisha,” alisema
Mama Amina.
Katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya watu kulikuwa
na burudani mbalimbali ambazo ziliongonzwa na Mshereheshaji maarufu wa eneo
hilo MC Mwajuma Nassoro na kusindikizwa
na nyimbo za kabila la wanyakyusa na Kigogo pamoja na msosi wa nguvu ulioandaliwa na wazazi wa watoto hao kwa kushirikiana na majirani.Watoto hao wakituzwa zawadi.
Catheline na Benjamin wakiwa na watoto wenzao kwenye sherehe hiyo.
Watoto wenzao nao wakijumuika kupata keki.
Catherine akilisha keko mama yake Bumi Heblon Mwaibale.
Benjamin akijiandaa kumlisha keki mama yake Bumi Mwaibale.
Mjomba Lusajo Mwaibale akilishwa keki. "Ni kama anasema keki tamu hii balaa"
Mama walezi wa watoto hao wakilishwa keki.
Mama wa watoto hao Lilian Hebron Mwaibale akijiandaa kulishwa keki.
Wageni waalikwa na ndugu, jamaa na marafiki wakijumuika pamoja kuserebuka.
Mserebuko ukiendelea.
Hapa ni sura zenye furaha tupu wakati wa sherehe hiyo.
Ni furaha tupu kwenye sherehe hiyo.
Catherine na Benjanin wakielekea eneo lililoandaliwa kwa sherehe hiyo.
Sherehe ikinogeshwa na vazi maalumu.
Sherehe ikiendelea.
Sherehe ikiendelea. Wageni waalikwa wakijumuika na familia ya Hebron Mwaibale kwenye sherehe hiyo.
Watoto wakiwa kwenye sherehe hiyo
Mjomba wa watoto hao Lusajo Hebron Mwaibale akiwapa zawadi wajomba zake.
Mama wa watoto hao Bumi Mwaibale (kulia) akiserebuka na rafiki zake katika sherehe hiyo.







No comments:
Post a Comment