Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Hashim Mgandilwa, akizungumza kwenye kikao cha kwanza cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga Desemba 6, 2025.
..........................................
Na Mashaka Kibaya, Kilindi
MKUU wa Wilaya ya Kilindi, Hashim Mgandilwa amewataka madiwani kuona umuhimu wa kusimamia miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao, iwe ile inayotekekezwa na fedha kutoka Serikali kuu na hata mapato ya ndani.
Ametoa rai hiyo juzi wakati alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha kwanza cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga.
Licha ya kuhimiza suala la usimamizi wa miradi,lakini pia Mgandilwa amewaomba madiwani kuemdelea kuwalea vyema watumishi kwa maelezo kuwa hao ndio wasaidizi katika utekezaji wa kazi zao.
Ametumia wasaa huo kuhimiza uwepo mahisiano mazuri baina ya madiwani, watumishi na wadau wa taasisi nyingine hatua aliyosema itasaidia kuchagiza uharakishwaji wa maendeleo wilayani.
Pia Mgandilwa hakusahau suala la maadili mema, akisema madiwani wanapaswa kuonekana wenye maadili mazuri wawapo kwenye utumishi na hata pale wanapokuwa nje ya kazi hiyo waliyoipata kwa kuaminiwa na umma.
"Unapokuwa kwenye nafasi lazima ufanane nayo, madiwani kwa nafasi mlizopewa nidhamu ni muhimu kuichunga, hayo ni maadili"alisema Mgandilwa akiwasisitiza madiwani kuwatumikia wananchi kwa yale watakayowatuma na amewaasa viongozi hao kutopandisha mabega.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya ya Kilindi amewashauri madiwani kuona umuhimu wa kujiweka karibu na makundi ya kijamii ili kuweza kupata taarifa mbalimbali kwa njia ya urahisi.
John Mgalula ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilindi, katika baraza hilo la madiwani alitumia fursa hiyo kusoma taarifa ya kazi zilizotekelezwa katika kipindi ambacho baraza la madiwani lilikuwa limevunjwa.
Vilevike aliwapongeza viongozi hao kwa kuaminiwa kuwa wawakilishi wa wananchi, ambapo kwa niaba ya watumishi aliahidi kushirikiana nao kwa kufanya kazi kwa karibu madiwani hao.
Katika kikao hicho cha madiwani mbali na viongozi hao wapya kuapishwa ili kuanza kuwatumikia wananchi, ulifanyika uchaguzi wa Mwenyekiti wa halmashauri na makamu wake, pia kamati ziliundwa na kupata viongozi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi, John Mgalula akizungumza kwenye kikao hicho.









No comments:
Post a Comment