Mchungaji Ester Mwasyoge Mwenyekiti wa Wilaya wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kaskazini Dodoma (kushoto), akiwa pamoja na Mchungaji Ephraim Mbise wa kanisa hilo Usharika wa Nkuhungu wakati wa ibada ya sakramenti ya kipaimara na ubatizo iliyofanyika Novemba 30, 2025 jijini Dodoma.
Na Dotto Mwaibale, Dodoma
WAZAZI wametakiwa kutenga muda wa kukaa na watoto ili
kuzungumza nao masuala mbalimbali ya maisha yakiwemo maadili jambo
litakalowasaidia katika maisha yao.
Ombi hilo limetolewa na Mchungaji Ester Mwasyoge Mwenyekiti
wa Wilaya wa Kanisa la Moravian Tanzania
Jimbo la Kaskazini Dodoma wakati akihubiri katika ibada ya sakramenti ya
kipaimara na ubatizo iliyofanyika Usharika wa Nkuhungu Novemba 30, 2025.a
“ Watoto wetu siku hizi wamekosa maadili kwa sababu wazazi
wengi wanashindwa kutenga muda wa kuzungumza nao baba akitoka saa 11 aljfajiri
akienda kwenye shughuli zake atarudi nyumbani saa nne usiku na kuwakuta
wamelala na wakati mwingine inaweza kupita hata siku tatu hajaonana nao,”
alisema Mwasyoge.
Alisema wazazi ndiyo wenye jukumu la kuwaelekeza watoto wao
miongozo ya maisha yao na hasa kuzigatia maadili, heshima, unyenyekevu na
masuala mengine yanayofanana na hayo yakiwemo
yanayohusu miili yao hasa kwa vijana walioingia kwenye umri wa kubalehe.
Akinukuu maneno ya Mungu kutoka Kitabu cha Kumbukumbu ya
Torati 6:4-9 ambayo baadhi yake yanasema Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako
wote na kwa roho yako yote na kwa nguvu zako zote.
“Na maneno haya ninayokuamuru leo yatakuwa katika moyo wako
nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii na kuyanena uketipo katika nyumba yako
na utembeapo njiani na ulalapo na uondokapo. Yafunge yawe dalili juu mkono
wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako, tena yaandike juu ya
miimo ya nyumba yako na juu ya malango yako,” Mchungaji Mwasyoge aliyanukuu maneno hayo kutoka katika
biblia.
Alisema maneno hayo ni ya muhimu na yanaimarisha upendo
baina ya watoto na wazazi na kuwa Mungu ni mmoja hakuna mwingine zaidi yake
anayepaswa kuabudiwa.
Mchungaji Mwasyoge aliongeza kuwa wazazi wanatakiwa
kuwafundisha watoto wao kuomba msamaha, kuhudhuria ibada za nyumbani na
kanisani, kuwafundisha stadi za kazi ili waweze kujitegemea na kutokwepa
majukumu yao.
Akisisitizia suala la maadili alisema watoto wengi hasa
vijana wamekuwa hawajielewe na ndiyo maana baadhi yao wamekuwa na mihemuko na
kufuata mikumbo na kujiingiza kwenye maandamano na hata wakiulizwa madai yao ni
yepi hawayajui.
Mwasyoge aliwataka watoto hao kuwasikiliza wazazi na walezi wao
na kuwatii na kueleza kuwa hivyo ndivyo Mungu anavyohitaji.
Katika hatua nyingine Mchungaji Mwasyoge aliwataka watoto
wote ambao wapo darasa la sita kuanza kujiandikisha kwa ajili ya kuanza mtaala
wa kipaimara badala ya kusubiri wakiwa darasa la saba kwani inakuwa vigumu
kutokana na kukabiliwa na maandalizi ya mitihani.
Aidha, aliutaka uongozi wa kanisa hilo Usharika wa Nkuhungu kutengeneza mpango kazi utakao saidia kuepusha mgongano wa tarehe wa matukio makubwa yanayofanyika katika kanisa hilo ili kutoa fursa na makanisa mengine kushiriki kwenye matukio husika.
Mchungaji Ester Mwasyoge Mwenyekiti wa Wilaya wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kaskazini Dodoma akihubiri katika ibada hiyo.
Mchungaji Ephraim Mbise wa kanisa hilo Usharika wa Nkuhungu Dodoma akisisitiza jambo katika ibada hiyo.
Watoto Benjamin Manase na Catherine Richard Skana wakiwa tayari kwenda kanisani kushiriki ibada hiyo.
Mtoto Benjamin Manase akiwa katika ubora wake kabla ya kupokea kipaimara
Mtoto Catherine Skana akiwa katika ubora wake kabla ya kupokea kipaimara.
Watoto wakiwa tayari kupokea kipaimara.
Watoto wakiwa katika ibada ya kupokea kipaimara.
Watoto wakiwa kwenye ibada hiyo. Kutoka kushoto ni Catherine Skana, Catherine Kefa, Florencea Mwasambili na Caroline Kefa.
Watoto hao wakionesha biblia baada ya kukabidhiwa.
Taswira ya ibada hiyo.
Waumini wakiwa kwenye ibada hiyo ya kipaimara.
Ubatizo kwa watoto ukifanyika.
Watoto waliobatizwa wakipata mbaraka.
Mtoto akikabidhiwa cheti chake baada ya kubatizwa.
Watoto wakiwa kwenye ibada hiyo. Kutoka kushoto ni Catherine Kefa, Catherine Skana na Jaqualine Nzowa.
Wana kwaya Kuu ya kanisa hilo Usharika wa Nkuhungu wakiwa kwenye ibada hiyo.
Watoto wa kipaimara wakiwa kwenye ibada hiyo.
Mtoto Benjamin Manase akipokea kipaimara.
Watoto wakiombewa wakati wa kupata kipaimara.
Mchungaji Ephraim Mbise akimpongeza mtoto Benjamin Manase kwa kupata kipaimara.
Watoto wakionesha furaha yao baada ya kupata kipaimara. Kutoka kushoto ni Catherine Kefa, Catherine Skana na Jaqualine Nzowa.
Mtoto Benjamin Manase akikabidhiwa cheti baada ya kupokea kipaimara.
Mtoto Stephano Nzowa akipongezwa na mdogo wake Moreen baada ya kupokea kipaimara.
Mtoto Catherine akikabidhiwa cheti baada ya kupokea kipaimara.
Watoto wakionesha vyeti vyao baada ya kupokea kipaimara.
Mtoto Catherine Kefa akivikwa shada na wazazi wake baada ya kupokea kipaimara.
Rose Michael (Maarufu Mama Elisafi) akimvika shada Mtoto Catherine Skana baada ya kupokea kipaimara.
Mtoto Denis Mwakilaba, akivikwa shada na mama zake wadogo baada ya kupokea kipaimara.
Mtoto Catherine Richard Skana, akiwa katika ubora wake baada ya kupokea kipaimara.
Christina Ndila akimpongeza mdogo wake Benjamin Manase baada ya kupokea kipaimara.







No comments:
Post a Comment