AKABIDHI PIKIPIKI KWA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII SINGIDA. - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, January 3, 2026

AKABIDHI PIKIPIKI KWA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII SINGIDA.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu akikabidhi pikipiki Nnae (8) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Singida zitakazisaidia kuwafikia jamii ya mkoa huo. Zoezi hilo limefanyika tarehe 02 Januari, 2026.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu akizungumza kabla ya kugawa pikipiki Nnae (8) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Singida zitakazosaidia kuwafikia jamii ya mkoa huo. Zoezi hilo limefanyika tarehe 02 Januari, 2026.
Baadhi ya maafisa Maendeleo ya Jamii wakimsikiliza  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu kabla ya kukabidhi pikipiki Nane (8) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Singida zitakazosaidia kuwafikia jamii ya mkoa huo. Zoezi hilo limefanyika tarehe 02 Januari, 2026.
Baadhi ya pikipiki Nane (8) zizlizotolewa na Wizaraya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Singida zitakazosaidia kuwafikia jamii ya mkoa huo. Zoezi hilo limefanyika tarehe 02 Januari, 2026
-------------------------------------------------------

Na Abdala Sifi - Singida 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kuhakikisha wanawafikia wananchi kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali na kuharakkisha maendeleo ya wananchi. 

Dkt Jingu amesema hayo leo tarehe 2 Januari 2026 Mkoani Singida wakati akikabidhi pikipiki nane (8) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii ambazo zinalenga kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi. 

“Maafisa Maendeleo ya Jamii ni viungo muhimu sana kati ya Serikali na wananchi, hivyo niwaombe mkazitumie hizi pikipiki kwa ajili ya kuwahudumia wananchi, kuwapa elimu ya fursa mbalimbali na kutatua changamoto zinazowakabili, kwa njia hiyo mtakuwa mmewasaidia kuongeza tija katika shughuli zao kwa maendeleo ya jamii”amesema Dkt Jingu. 

Aidha Dkt. Jingu amesema Serikali  inayooongozwa na Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  inatambua umuhimu wa Maafisa Maendeleo ya Jamii, hivyo itaendelea kuhakikisha inawapatia vitendea kazi ili kutekeleza majukumu yao ipasavyo. 

Dkt.Jingu amewasihi Maafisa hao kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali, kuhakikisha kila mwanachi anazitambua fursa hizo na kumwezesha kuziendea kwa ajili ya maendeleo yao. 

Amezitaja baadhi ya fursa hizo ni pamoja na mikopo kwa wafanyabiashara ndogondogo, uwezeshaji wanawake kiuchumi pamoja na fursa nyingine zinazotolewa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo. 

Kwa upande wake Afisa Maendeleo wa Mkoa wa Singida Patrick Kisango ameishurkuru Serikali kwa kuwapatia Maafisa Maendeleo ya Jamii pikipiki hizo na kwamba zitarahisisha utendaji wa kazi na kuharakisha maendeleo kwa wananchi. 
2022/23 hadi 2024/25, imetoa pikipiki (208) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii katika mikoa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad