Afisa Mahusiano , Ramadhani Nyamugumi (mwenye t-shirt nyeusi) akizungumza na wateja waliotembelea banda la benki hiyo kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma za kifedha yalioandaliwa na serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango yaliyofanyika Usagara jijini Tanga.
............................
Na Mwandishi Wetu, Tanga
Bank of Africa Tanzania ilivyoshiriki wiki ya huduma za kifedha kitaifa
Bank of Africa Tanzania imeshiriki katika maadhimisho ya wiki ya Huduma ya Kifedha yaliyoandaliwa na Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango yaliyofanyika katika viwanja vya Usagara vilivyopo jijini Tanga.
Yakiwa na kauli mbiu isemayo “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi,” malengo makuu ya maadhimisho hayo yalikuwa ni kuongeza uelewa, kuboresha ufahamu na hatimaye kuhamasisha mabadiliko ya tabia za wananchi katika usimamizi wa fedha na matumizi ya huduma rasmi za kifedha.
Aidha, tukio hilo lililenga kuwahamasisha Watanzania kutumia huduma rasmi za kifedha kama sehemu ya jitihada za kupunguza kiwango cha umaskini katika jamii, ili kufikia maendeleo ya kiuchumi jumuishi na endelevu.
Afisa Mahusiano , Ramadhani Nyamugumi (kushoto mwenye t-shirt nyeusi) na Gilber John ambaye pia ni Afisa Mahusiano wa Benki hiyo wakitoa ufafanuzi na maelezo jinsi bneki hiyo inavyofanya kazi nchini katika maadhimisho ya wiki ya huduma za kifedha yaliyofanyika Usagara jijini Tanga.










No comments:
Post a Comment