RAS SINGIDA AONGOZA UKAGUZI WA MIRADI YA ELIMU, AFYA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Wednesday, 28 January 2026

RAS SINGIDA AONGOZA UKAGUZI WA MIRADI YA ELIMU, AFYA

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Fatma Mganga, akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa miradi ya elimu na afya  katika katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Januari 28, 2026.

.............................................

Na Mwandishi Wetu, Singida. 

Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Fatma Mganga amefanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya elimu na afya vilevile kuhakikisha matumizi sahihi ya fedha za umma huku akiwataka wazazi na viongozi kuhakikisha watoto wanapata haki yao ya Elimu na kushiriki kikamilifu katika Mpangilio wa Lishe.

Katika ziara hiyo, Dkt. Mganga akiiongoza timu ya ukaguzi amekagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Zahanati ya Kitongoji cha Mlongoji, unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na wananchi.

Serikali Kuu imetoa Tsh 50,000,000 kwa ajili ya umaliziaji wa zahanati hiyo, huku wananchi wakichangia Tsh 2,614,000, wadau Tsh 2,750,000 na nguvu kazi yenye thamani ya Tsh 1,250,000. Aidha, Mfuko wa Jimbo ulitoa Tsh 10,000,000 na hadi sasa, jumla ya Tsh 13,437,815.51 tayari imetumika.

Kwa upande wa miradi ya elimu miradi iliyokaguliwa, ni pamoja na ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa katika Shule ya Msingi Kitaraka unaofadhiliwa kupitia Programu ya BOOST kwa gharama ya Tsh 92,000,000. 

Miradi ya elimu iliyokaguliwa, ni pamoja na ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa katika Shule ya Msingi Kitaraka.

Hadi sasa Tsh 69,055,299 tayari zimetumika. Mradi huo unatarajiwa kunufaisha wanafunzi 667. Katika Shule ya Msingi Kazikazi, kamati ilikagua ujenzi wa madarasa ya awali na msingi pamoja na matundu ya vyoo, mradi unaogharimu Tsh 120,000,000 kupitia Programu ya BOOST.

Aidha katibu tawala huyo ameongoza timu yake hiyo ya ukaguzi aliyoambatana nayo kukagua mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Msingi ya Kijobolo iliyopo Kitongoji cha Milumbi, unaotekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali na wananchi. 

Mradi huo umefadhiliwa na michango ya wananchi, Mfuko wa Jimbo, Halmashauri ya Wilaya ya Itigi na Programu ya BOOST kwa jumla ya zaidi ya Tsh 300,000,000, ambapo hadi sasa zaidi ya Tsh 214,000,000 tayari zimetumika. 

Dkt. Fatma Mganga na timu yake wakiendelea na ukaguzi wa miradi.
 
Chanzo Jambo FM.

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad