Timu hiyo ya Shule ya Sekondari ya Magnus
.....................................
Na Mwandishi Wetu.
BAADA ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika michuano ya Afrika Mashariki na Kati maarufu Feassa, mchezaji wa mpira mikono wa Shule ya Sekondari ya Magnus iliyoko Pugu, jijini Dar es Salaam, Bakar Omary amechaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu Cha Kampala, nchini Uganda.
Michuano hiyo inayoshirikisha vijana chini ya miaka 20, iliyofanyika mwaka Jana, ambapo Omary alipata ufadhili wa kusoma katika Chuo Cha Kampala kwa lengo la kuendeleza kipaji chake.
Katika michuano hiyo, iliyoshirikisha nchi za Ethiopia, Burundi, Uganda, Ivory Coast, Kenya na Tanzania, wanafunzi wanne Shule ya Sekondari ya Magnus walichaguliwa kwenye kikosi cha Taifa. cha Tanzania kwa ajili ya kushiriki Feassa.
Wachezaji kutoka Magnus waliochaguliwa kujiunga na kikosi cha Taifa ni pamoja na Wahab Juma, Idrisa Ngembe, Birad. Ramadhan na Omary.
Akizungumza shuleni hapo, mwalimu wa michezo wa Shule ya Magnus, Dislasi Kenyanya, alisema wamekuwa na program ya kuibua vipaji chipukizi kwa lengo la kuwaendeleza.
Kenyanya alisema pamoja na shule kufundisha masomo mengine, lakini michezo wanaipa kipaumbele kwa kuwa ni sehemu ya ajira kwa vijana.
Alisema kwa sasa michezo ni ajira kubwa duniani, pia inawasaidia wanafunzi kujenga afya ya akili.
"Sisi hapa shuleni tunafundisha michezo kama soka, netiboli, wavu na mpira wa mikono," alisema Kenyanya.
Mwalimu huyo alisema kutokana na uwezo mkubwa wa kucheza, kijana wao, Omary mwaka jana alipata ufadhili wa kusoma Kampala baada ya kuonyeaha kipaji cha hali ya juu katika michuano ya Feassa.
Ametoa wito kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwenda shuleni hapo kwa ajili ya kuangalia vipaji.
Pia amewaomba wazazi kuwapeleka watoto wao katika Shule ya Magnus ili waweze kupata eiimu bora.







No comments:
Post a Comment