Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 49 tangu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Februari 5, 1977 yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), yaliyofanyika Januari 26, 2026 wilayani Ikungi mkoani Singida.
......................
Na Dotto
Mwaibale, Singida
MBUNGE wa
Jimbo la Ikungi Mashariki Mhe. Thomas Mgonto ameendelea kuchanja mbuga kwa kuwapelekea
maendeleo wananchi wa jimbo hilo katika nyanja tofauti ambapo awamu hii ameigusa
sekta ya elimu kwa kutoa vifaa vya michezo kwa Shule za Sekondari ya Mungaa na Makiungu.
Hafla ya
kukabidhi vifaa hivyo ni moja ya tukio katika kuadhimisha miaka 49 tangu kuzaliwa kwa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Februari 5, 1977 yaliyofanyika wilayani Ikungi mkoani Singida Januari 26, 2026.
Maadhimisho
hayo yalifanywa na Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho Wilaya ya Ikungi chini ya
Mwenyekiti wake Haji Kangaa ambaye alimwakilisha mbunge huyo aliyekuwa mgeni
rasmi lakini hakuweza kushiriki kutokana na kuwa na majukumu mengine ya kikazi.
Mkangaa
akizungumza katika maadhimisho hayo aliwahimiza wanafunzi wa shule hizo kusoma
kwa bidii, kuwa na nidhamu ili waweze kutimiza ndoto za maisha yao pamoja na
kuwa viongozi wa baadae.
Aidha,
Kangaa aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha
wanawapeleka watoto wao shuleni kwani ni haki yao ya msingi ya kupata elimu na
hivyo kusiwepo na vikwazo vyovyote wakati wa kuwandikisha na hata kama
hawatakuwa na sare za shule na mahitaji mengine wapokelewe.
Vifaa hivyo
vya michezo vilikabidhiwa na Katibu wa mbunge huyo Hussein Mseule ni jezi na
mipira.
Wajumbe wa
Jumuiya hiyo walimshukuru na kumpongeza Mhe. Mgonto kwa jitihada zake
anazozifanya za kuwatumikia.
Kwa upande
wao wanafunzi wa shule hizo walimshukuru mbunge huyo kwa kuwapa vifaa hivyo
ambavyo vitasaidia kuibua vipaji vya michezo.
Katika maadhimisho hayo zilifanyika shughuli zingine za kijamii ikiwemo kupanda miti ikiwa ni kumuunga mkono Rais wa Jamhuri yaa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye Januari 27, 2026 amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kupanda miche ya miti nyumbani kwake Kizimkazi Zanzibar.
Viongozi wakiwaa mezaa kuu wakati wa maadhimisho hayo.
Mwenyekiti waa Jumuiya yaa Wazazi Wilayaa ya Ikungi, Haji Kangaa aakizungumza na wanafunzi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Wilaya ya Ikungi, Haji Kangaa akiongoza shughuli ya kupanda miti.
Vifaa vya michezo vikikaabidhiwa.
Vifaa vya michezo vikikaabidhiwa.














No comments:
Post a Comment