Mchungaji Mpina Bahara.
..................................
Na Mwandishi Wetu.
MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Assemblies of God (TAG), lililoko Tandika Maghorofani, jijini Dar es Salaam, Mpina Bahara, amesema kwamba wanatarajia kuandaa semina ya ujasiriamali kwa waumini wao wakiwamo wajane na yatima ili kuwainua kiuchumi.
Akizungumza baada ya misa ya ibada iliyofanyika juzi Jumapili, Mchungaji Bahara alisema kanisa lake limeweka mipango mingi kwa mwaka huu.
Mchungaji Bahara alisema mipango yao ya mwaka huu waliyo nayo ni pamoja kuandaa mikutano minne mikubwa ili kufikia dira na malengo waliyojiwekea.
Alisema kuwa mpango mwingine waliojiwekea ni kuandaa semina kwa wajane, yatima na walio katika mazingira magumu ili kuwakwamua kiuchumi.
"Huwezi kuongoza watu ambao hawana kipato ni mzigo kwa kanisa," alisema Bahara.
Bahara alisema semina itakayoandaliwa kwa wajasiliamali hao itasaidia kuongeza uchumi wao.
Pia Mchungaji huyo, alisema kanisa linampango wa kuanzisha ibada ya pili ambayo itahubiliwa kwa Lugha ya Kiingereza ili kuyafikia mataifa yote.
Alisema mipango yao mingine ni kuanzisha programu ya masela Church kwa lengo la kuyafikia makundi maalumu ya vijana yaliyoathirika na matumizi ya dawa za kulevya.
Alisema wataunda timu maalumu ya kufanikiwa kufika katika mazingira yanayokaliwa na makundi hayo ya vijana ili kuwapa elimu na baadaye waweze kuachana na tabia ya kutumia dawa za kulevya.







No comments:
Post a Comment