NAIBU SPIKA KIONGOZI WA VITENDO MWENYE KASI YA KUWATUMIKIA WANANCHI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, January 3, 2026

NAIBU SPIKA KIONGOZI WA VITENDO MWENYE KASI YA KUWATUMIKIA WANANCHI

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Mhe. Daniel Sillo (wa pili kushoto), akipokea taarifa alipokuwa kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa baadhi ya shule katika jimbo hilo.

.............................

Na Dotto Mwaibale

KIONGOZI bora ni yule anayefanya kazi kwa vitendo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na siyo kukaa ofisini na kuagiza wakuu wa idara au wasaidizi wake.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Mhe. Daniel Sillo hakika ni kiongozi wa vitendo zaidi mwenye kasi ya kuwatumikia wananchi.

Kutokana na kufanya kazi kwa ratiba kasi ya utendaji wake inaongezeka kila siku ambapo jana Januari 3, 2026, alifanya ziara ya kikazi katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Manyara pamoja na Shule ya Sekondari Kisangaji, kwa lengo la kukagua hatua iliyofikiwa katika ukamilishaji wa mabweni ya wanafunzi wa kike na wa kiume katika shule hizo.

Katika ziara hiyo, Mhe. Sillo alikagua maendeleo ya ujenzi wa mabweni yaliyogharimu jumla ya Sh. Milioni 260 shule ya sekondari Kisangaji, fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuishi wanafunzi.

Mhe. Sillo aliridhishwa na matumizi ya fedha hizo pamoja na ubora wa kazi uliofanyika, akisisitiza umuhimu wa kusimamia miradi ya maendeleo kwa uadilifu na thamani halisi ya fedha.

Aidha, alitembelea Shule ya Sekondari ya Wavulana Manyara, mradi mkubwa wa elimu unaogharimu Sh. Bilioni 4.1. 

Ameeleza kuwa kwa sasa wanafunzi wa kidato cha tano tayari wanaendelea na masomo, huku wanafunzi wa kidato cha kwanza wakitarajiwa kuanza masomo mwezi huu, hatua inayodhihirisha dhamira ya Serikali ya kuimarisha elimu ya sekondari katika Mkoa wa Manyara.

Akizungumza na walimu na viongozi wa elimu, Mhe. Sillo amewahimiza watendaji kuhakikisha wanakamilisha miradi kwa wakati na kuitunza miundombinu iliyopo ili idumu kwa muda mrefu.

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Mbunge huyo kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Jimbo la Babati Vijijini, hususan ya sekta ya elimu.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Mhe. Daniel Sillo (wa tatu kushoto), akizungumza na wataalam na viongozi mbalimbali wakati wa ziara hiyo.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Mhe. Daniel Sillo (katikati nyuma) akiwa katika picha ya pamoja na wataalam na viongozi mbalimbali baada ya ziara hiyo.

Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale namba ya simu 0754362990.


 Chanzo cha habari ni HW-NEWS

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad