...................................
MWENYEKITI na Mkurugenzi Mkuu wa SSI Group & SS Foundation, Dk. Yasini Bakari, amesema wanatarajia kuzindua Mpango wa Taifa wa Damu Salama utakaofanyika Jumamosi ijayo, Kivule, Ilala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini, Dk Bakari alisema mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa kushirikiana na SSI ARJA na SSI Foundation itazindua operesheni ya majaribio, ambapo siku hiyo itakuwa uzinduzi rasmi wa kitaifa.
Katika uzinduzi huo utakaofanyika Kivule, matarajio yao ni kuwa kukusanya chupa 600 za damu.
Wiki iliyopita SSI Group kwa kushirikiana na Kikundi cha UWEZO COMMUNITY MICROFINANCE GROUP walikusanya damu chupa zaidi ya 30 wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa UWEZO uliofanyika Kivule, jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo, SSI Group ambao walikuwa wageni waalikwa, Dk Bakari aliwapongeza UWEZO kutokana na jinsi wanavyofanya kazi zao kwa umakini, lakini wanachama wao waliojitoa kuchangia damu.
Dk Bakari alisema watu wanatakiwa kujitolea damu ili kuokoa maisha wenzetu ambao wanahitaji damu kutokana na magonjwa mbalimbali.
Pia wamewataka wananchi kujitokea siku ya uzinduzi rasmi wa Mpango wa Damu Salama ambao utahudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali.







No comments:
Post a Comment