WAFANYAKAZI BODI YA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI WAPIGA KAMBI YA KIKAO KAZI SINGIDA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, January 15, 2026

WAFANYAKAZI BODI YA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI WAPIGA KAMBI YA KIKAO KAZI SINGIDA

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kufungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi mkoani Singida Januari 15, 2026.

.....................

Na Mwandishi Wetu, Singida

WAFANYAKAZI wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB)wamekutana mkoani Singida katika kikao cha baraza la wafanyakazi kwa ajili ya kuweka mikakati ya pamoja namna ya kujadili utendaji wa kazi.

Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB, Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari wakati akifungua kikao hicho Januari 15, 2026 alisema watakuwepo kwa siku mbili mkoani Singida kwa ajili ya kujadili mpango kazi wa kitaasisi pamoja na kufanya tathimini ya utendaji ya mwaka uliopita na kuweka mkakati wa pamoja wamaboresho katika idara mbalimbali na vitengo.

“Tunafanya kikao hiki ili tuweze kuendana na sheria inayotuongoza kutekeleza majukumu yetu mbalimbali ya Serikali,” alisema Mbanyi.

Mbanyi alisema baraza hilo la wafanyakazi huwa linafanyika mara mbili na ni chombo cha kiuwakilishi na kuwa katika kikao hicho kuna wakuu wa idara na vitengo vyote na kila kitengo kimetoa mwakilishi mmoja mmoja wa kusikiliza na kuwasilisha mijadala ambayo wataona inafaa kwa maboresho ya utendaji katika maeneo yao.

Alisema katika taasisi za Serikali mabaraza hayo ya wafanyakazi yapo kwa mujibu wa sheria ya mahusiano kazini na katika usimamizi wa ujumla wa kitaifa wapo chini ya ofisi ya waziri mkuu.

“Katika kikao hiki tutajadili utendaji wa nusu mwaka katika mwaka huu wa fedha wa 2025/ 2026 tuangalie tumefanya nini wakati tukijielekeza mwaka mpya wa fedha wa 2026/2027 na kuangalia maboresho zaidi na kuona tunaendaje,” alisema Mbanyi.

Alisema katika kikao hicho pia watasikiliza maoni ya wafanyakazi ambao hawapo kwenye vikao vya maamuzi na kuyapeleka kwenye vikao vya menejimenti kwa ajili ya kuyafanyia kazi.

Kwa upande wake mwakilishi wa vijana wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) katika bodi hiyo, Seif Musa alisema katika kikao hicho wanatarajia makubwa kwa yale watakayoyajadili na kuelekezwa na kufuata miongozo mbalimbali itakayopendekezwa.

Naye Nancy Mwamakimbula Msimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala PSPTB amesema kupitia baraza hilo wanategemea kupata maoni mengi ya wafanyakazi ya kuboresha utendaji wa kazi.

Alisema katika baraza hilo pia watazungumzia masuala ya bajeti na maoteo ya bajeti ya mwaka ujao wa 2026/ 2027 pamoja na utekelezaji wake.

“Kimsingi tunatarajia baraza hili kuwa na manufaa sana kwetu hasa katika maboresho ya utendaji kazi na kuboresha mambo yote ambayo watumishi wote watatamani yaboreshwe yanayohusu taasisi na taaluma ya Ununuzi na Ugavi nchini. Mwenyekiti  wa  Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE), Tawi La PSPTB-Dodoma. Shilla Mwandu akizungumza.

Mwakilishi wa Vijana. Tawi La PSPTB- Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) Dodoma Seif Mussa akizungumza
Afisa Rasilimali  Watu na Utawala PSPTB, Nancy  Mwamakimbula akizungumza
Kikao kikiendelea
Picha ya pamoja
Wakiimba wimbo wa mshikamano wa Wafanyakazi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad