Na Issa Mwadangala.
Wananchi wa Kijiji cha Chumbageni kata ya Isongole wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe wametakiwa kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pindi wanapobaini viashiria au matukio ya uhalifu katika maeneo yao, ili watuhumiwa washughulikiwe kwa mujibu wa sheria za nchi.
Elimu hiyo ilitolewa Januari 31, 2026 na Polisi kata wa kata hiyo Mkaguzi wa Polisi Milton Mponzi, ambapo aliwasitiza umuhimu wa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa mapema, jambo litakalosaidia kudumisha amani, utulivu na haki katika jamii.
Mnatakiwa kuhakikisha mnaishi na kushiriki kikamilifu katika miradi ya Polisi Jamii kama vile Familia Yangu Haina Mhalifu, pamoja na kupinga vitendo vya wizi kwa vitendo kwa kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi vitakavyosaidia kukomesha uhalifu na kuimarisha usalama katika jamii yao" alisema Mkaguzi Mponzi.
Jeshi la Polisi kupitia Polisi Kata linaendelea kuwahimiza wananchi kushirikiana nalo kwa karibu kwa kuzingatia sheria, kutoa taarifa kwa wakati na kulinda amani ya nchi, kwani usalama ni jukumu la kila mmoja wetu.

.png)






No comments:
Post a Comment