TOENI TAARIFA ZA WAGENI KUIMARISHA USALAMA - SINGIDANI BLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, 1 February 2026

TOENI TAARIFA ZA WAGENI KUIMARISHA USALAMA

Na Issa Mwadangala.

Wakazi wa Kitongoji cha Saza Kati, Wilaya na Mkoa wa Songwe, wametakiwa kushirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wageni, hususan wanaohamia na kuishi katika maeneo yao, ili kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

Akitoa wito huo Januari 31, 2026, Polisi Kata wa Mkwajuni, Mkaguzi wa Polisi Stela Rwekamwa, amesisitiza kuwa ushirikiano wa wananchi ni nguzo muhimu katika kulinda amani, akiahidi kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuchukua hatua stahiki kwa taarifa zote zitakazotolewa kwa wakati.

Mkaguzi Stela, alisisitiza umuhimu wa kila mgeni anayehamia eneo hilo kujulikana rasmi kwa Balozi wa eneo husika, hatua inayolenga kudhibiti uhalifu, kuzuia vitendo viovu na kuweka mazingira salama kwa jamii, huku akiwakumbushwa wakazi hao kuwa usalama unaanza na wao wenyewe kwa kutoa taarifa mapema bila hofu ili Jeshi la Polisi liweze kuzishughulikia kwa haraka.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad