Je, unaweza kufikiria kurudi pale ulipopaki gari lako na kukuta
nafasi iko wazi kabisa? Hakuna vioo vilivyovunjwa, hakuna alama ya kuvutwa, ni
pengo tu linalokuangalia kama kejeli. Hilo ndilo lililompata Samuel,
mfanyabiashara wa vifaa vya simu katika mtaa wa Rongai, ambaye alipoteza gari
lake mchana kweupe lakini akalipata kwa njia iliyowaacha wengi wakishangaa.
Samuel alikuwa ameegesha gari lake nje ya maduka ili apeleke
mzigo kwa mteja. Hakukaa hata dakika ishirini. Aliporudi, alipiga hatua mbili
mbele kisha akasimama. Alidhani amechanganya sehemu. Aliangalia kulia na
kushoto. Hakukuwa na gari lake.








No comments:
Post a Comment