Katibu wa Mbunge huyo, Hussein Mseule akuke Hussein Mseule akishiriki kupanda miti
............................................
Na Dotto Mwaibaale, Singida
MBUNGE wa Jimbo la Ikungi Mashariki Mhe. Thomas Mgonto amejidhihirisha kuwa hapoi ambapo pamoja na kufanya shughuli za kijamii kuadhimisha miaka 49 ya Chama cha Mapinduzi (CCM) tangu kuzaliwa kwake Februari 2, 2026 ametumia maadhimisho hayo kusikiliza kero za wananchi.
Kutokana na moto wake wa utendaji kazi hata akiwa nje ya jimbo hilo amekuwa akiwakirishwa vizuri na Katibu wake Hussein Mseule kutekeleza majukumu yake.
Katika maadhimisho hayo Wananchi na wana CCM wa Kata ya Dung’unyi na Kijiji cha Kipumbuiko wakiongozwa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Dung’unyi, Paul Mbano na Rosemary Zakaria ‘ Sweetbert walishiriki kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kipumbuiko iambayo ujeni wake unatarajia kuanza hivi karibuni kwa nguvu za wananchi.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa wa CCM Wilaya yaa Ikungi ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yaliyofanyika Februari 4, 2026 uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo pamoja na upandaji miti.
Kutokana na ufanyaji kazi kwa kushirikiana na kufuata maelekezo ya mbunge huyo Katibu wake Hussein Mseule alitumia nafasi hiyo kusikiliza kero za wananchi ambazo aliziwasilisha kwa mbunge wake kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
“Siku zote huwa nafanya kazi kwa ratiba iliyopangwa na mbunge wetu Chifu Mgonto na ndiyo maana leo nilikutana na wananchi na kusikiliza kero zao ambazo tayari nimeziwasilisha ofisini kwake,” alisema.
Miti ikipandwa.
Msingi wa nyumba ukichimbwaKazi ikiendelea















No comments:
Post a Comment