......................................
Na Dotto Mwaibale, Singida
RATIBA ya kazi ni mpangilio maalumu wa muda na shughuli zinazotakiwa kufanywa ndani ya kipindi fulani ili kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa ufanisi.
Kufanya kazi kwa ratiba inasaidia kupanga vipaumbele, kuongeza tija, kuzuia kusahau majukumu, na kuhakikisha muda wote unatumika kwa shughuli zenye tija.
Faida kuu za kuwa na ratiba ya kazi ni kuweka vipaumbele na huondoa mambo yasiyo ya msingi na kuzingatia yale ya muhimu.
Baadhi ya mambo hayo ni kuongeza ufanisi, hutoa mwongozo wa nini cha kufanya na kipi kinafuata, husaidia kukumbuka majukumu yote kwa kuyaorodhesha na huhakikisha muda hautumiki vibaya.
Katika muktadha wa elimu, ratiba ya kazi pia inaweza kumaanisha mpangilio wa mada, shughuli za ujifunzaji, na tathmini zinazopaswa kufundishwa kwa kipindi maalumu.
Moja ya faida za kuwa na ratiba ni vigumu kupata muda ambao haujapangiwa jukumu au kazi kwenye ratiba.
Mbunge wa Jimbo la Itigi mkoani Singida Mhe.Yohana Msita ni mbunge anayefanya kazi yake kwa kufuata ratiba jambo ambalo linamrahisishia utekelezaji wa mipango yake ya kazi.
Kesho Februari 17, 2026 Mhe. Msita anaanza ziara ya kutembelea shule mbalimbali katika jimbo hilo ili kujua changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi.
Kwa mujibu wa ratiba aliyoiandaa kuanzia Saa 2:00-3:20 asubuhi atakuwa Shule ya Msingi Mlandizi na kisha atakwenda Shule ya Itigi Majengo Sekondari ambapo atawasili Saa 3:30 hadi – Saa4:50 asubuhi.
Baada ya hapo Mhe. Msita Saa 5:00-6:25 mchana atakuwa Sekondari ya Handu ambapo atafanya kikao na Watumishi wa shule hiyo kitakachoanza saa 6:30-7:45 mchana na baadae kumalizia ziara hiyo Shule ya Sekondari ya Kimadoi itakayoanza saa 8:00-9:30 Alasiri.
Kwa mujibu wa ratiba malengo la ziara hiyo ni kuzungumza na walimu, pamoja na wanafunzi wa madarasa ya mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne kwa ajili kuhamasisha na kuinua ari ya ufaulu.








No comments:
Post a Comment