MGONTO MBUNGE MWENYE SHUKRANI, AANZA KAZI VIZURI - SINGIDANI BLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Tuesday, 10 February 2026

MGONTO MBUNGE MWENYE SHUKRANI, AANZA KAZI VIZURI

Mbunge wa Jimbo la Ikungi Mashariki, Mhe. Thomas Mgonto (Mwenye Skafu), alipokuwa akikabidhi mfano wa hundi ya mikopo ya silimia 10 iliyotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Desemba 23, 2025 kwa ajili ya Vikundi vya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu.

.......................................... 

Na Dotto Mwaibale, Dodoma

SHUKRANI ni hali ya kurudisha hisia chanya kwa mema au mabaya yaliyokufikia.

Kwa tafsiri ya kidunia, shukrani inatolewa pale mtu anapopokea mambo mema Kwamfano mtu atarudisha shukrani aidha ya maneno au matendo pale anapozawadiwa kitu, au anapofanyiwa jambo fulani jema.

Lakini katika maneno ya Mungu (Biblia au Quran), Shukrani inatolewa si tu baada ya kupokea mambo mazuri na mema bali pia kwa mambo yote mazuri na mabaya.

Maana ya shukrani ni lazima kumshukuru Mungu hata katika yale mambo ambayo tunaona hayajaenda kama tulivyotarajia,

Tuna amini kuwa mambo yote mabaya na mazuri yanayotokea tunajua ni mapenzi ya Mungu kwa wote waliondani ya dini na ni vizuri kumshukuru Mungu kwa mema anayotufanyia.

Moyo wa shukrani ni moyo unaompendeza Mungu na moyo usio na shukrani huondoa mema yote na Baraka zote kwetu kutoka kwa Mungu.

Baadhi ya watu wanajifungia milango yao ya Baraka baada ya kukaa kimya pale wanapotendewa jambo fulani na Mungu, lakini wengine wanaendelea kujifungulia  milango ya Baraka  baada ya kumshukuru Mungu kwa mambo waliyotendewa.

Shukrani ni jambo linalompendeza Mwenyezi Mungu na linaloendeleza Baraka kwa kila mtu ambaye anajua kutoa shukrani.

Lengo la kuanza kutoa  ufafanuzi kuhusu shukrani ni kutaka kumzungumzia Mbunge wa Jimbo la Ikungi Mashariki Mhe. Thomas Mgonto (Maarufu kama Chifu Mgonto).

Mbunge huyu ni mwanasiasa kabla ya kupata nafasi hiyo alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida kwa kipindi cha miaka mitano 2020/ 2025 ambapo alijitokeza kuwania nafasi hiyo kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025 na kuibuka kidedea.

Mhe. Mgonto baada ya kupata nafasi hiyo alipanga ratiba ya kupita kwa wananchi kwenda kutoa shukrani kwa kumchagua jambo ambalo ni kubwa mbele ya Mungu na Wanadamu.

Kuna baadhi ya watu hata wakifanyiwa mambo mema kiasi gani wanashindwa kabisa kushukuru wakiona ni haki yao kufanyiwa hivyo baada ya Mwenyezi Mungu kuwapa neema waliyo nayo ambayo anaweza kuwanyang’anya wakati wowote akiamua kufanya hivyo.

Katibu wa  mbunge huyo Hussein Mseule amesema kuwa baada ya kuapishwa Mhe. Mgonto aliandaa ziara maalumu ya kwenda kutoa shukrani kwa wananchi sanjari na kusikiliza kero zao.

Alisema alifanya ziara hiyo kwa kutembelea kata tano na vijiji 15 vilivyopo kwenye jimbo hilo ambapo pia alikukutana na kamati ya siasa ya Wilaya ya Ikungi na kuishukuru kwa kazi kubwa iliyofanya nakufanikisha kupatikana kwa ushindi na kuelezea dira yake ya kazi. .

Mseule alisema baada ya kuonesha moyo huo wa shukrani kwa wananchi na mbele ya Mungu kuna kazi kadhaa alizozifanya na kuonesha safari yake njema aliyoianza ya kuwatumikia wananchi baada ya kuchaguliwa.

Alisema moja ya tukio lake kubwa la kwanza alilolifanya ni kukabidhi gari la wagojwa katika Kituo cha Afya cha Kata ya Ntuntu tukio ambalo lilivuta hisia za watu wengi.

“Tukio hilo liliwavutia watu wengi ambao walisema mbunge wao ameanza kazi vizuri ya kuwatumikia na kuwa gari hilo linakwenda kuwapunguzia adha waliyokuwa nayo pale wagonjwa waliohitajika kupelekwa hospitali kubwa kupata huduma hasa wajawazito na watoto,” alisema Mseule.

Mseule alisema tukio lingine alilolifanya mbunge huyo aliyekuwa mgeni rasmi ni kukabidhi fedha za mikopo ya asilimia 10 zilizotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Mseule aliongeza kuwa kuna kazi nyingine aliyoifanya ya  kuifanyia maboresho makubwa kwa siku mbili eneo la Sie katika barabara ya Mungaa kwenda Lighwa baada ya kupokeo kero hiyo kutoka kwa wananchi.

Aidha, Mseule alisema mbunge Mgonto ana mipango mizuri ya kuwatumikia wananchi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na jumuiya zake bila ya kuitaja mipango hiyo.

Hafla ya kukabidhiwa gari la wagonjwa ikiendelea.
Mbunge Mgonto akiwa katika kumtano wa kushukuru wananchi wa Kata ya Dung'unyi kwa kumchagua.
Mhe. Mgonto akijaribu kuwasha gari la wagonjwa ikiwa ni ishara ya kulikabidhi Kituo cha Afya cha Ntuntu katika hafla iliyofanyika Januari 4, 2026 wilayani humo.
Mbunge Mgonto akikata utepe kuashiria kukabidhi gari la wagonjwa Kata ya Ntuntu.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kuwasilisha kero zao kwa mbunge wao ili zifanyiwe kazi. 

Makala hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale namba ya simu 0754362990.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad