Naitwa Jackson, mzaliwa wa mkoa wa Mara lakini nimeishi Dar es Salaam kwa miaka kumi sasa. Nilimaliza elimu yangu ya juu nikiwa na matumaini makubwa ya kupata kazi ya maana na kuikwamua familia yangu kutoka kwenye lindi la umaskini. Lakini ndugu zangu, maisha ya jijini Dar yalinionyesha cha mtema kuni.
Kwa miaka sita, nilikuwa nikizungusha bahasha za ‘CV’ kila ofisi, kuanzia Posta hadi mitaa ya Mikocheni, lakini majibu yalikuwa ni yale yale: “Tutakupigia.”
Soli za viatu vyangu zilimalizika, na nikaanza kuonekana kichekesho mtaani. Watu walianza kunidhihaki wakisema elimu yangu haina faida, na hata marafiki zangu wa karibu walianza kunikwepa wakihofia kuwa nitaomba hela ya kula. Nilikuwa nimekata tamaa kabisa, nilihisi kama kuna giza nene limefunika kichwa changu kiasi kwamba waajiri walikuwa hawaoni uwezo wangu.








No comments:
Post a Comment