Prof. Shemdoe alifanya mazungumzo hayo na
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Benki ya Azania tarehe 05 Februari 2026 ofisini
kwake Jijini Dodoma, alipomtembelea kwa lengo la kujitambulisha ili kujenga
mahusiano mazuri ya kiutendaji yatakayowanufaisha wananchi waliopo kwenye
Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Katika kikao kazi hicho, Prof. Shemdoe na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Bi. Esther Mangenya wamekubaliana
kujenga mahusiano mazuri ili wananchi wanufaike na mchango wa Serikali na benki
hiyo katika kuboresha miundombinu ya utoaji wa huduma za kijamii.
Kwa kutambua mchango wa taasisi za kifedha kwa
jamii, Prof. Shemdoe amesema ofisi yake ipo tayari kushirikiana na benki hiyo
na kuitambulisha katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili waifikie jamii na
kuihudumia.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
Azania Bi. Esther Mangenya amemueleza Prof. Shemdoe kuwa benki yake imedhamiria
kuwajibika kwa jamii kwa kutoa mchango utakaoboresha huduma mbalimbali za
kijamii ikiwepo na za kifedha.
Prof. Shemdoe tangu apewe dhamana na Mhe. Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kusimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa, amekuwa
mstari wa mbele katika kukutana na Wadau wa Maendeleo kwa lengo la kuboresha
ushirikiano na ofisi ili kupeleka tabasamu kwa wananchi na ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amekutana
na Mkurugenzi mtendaji Benki ya Azania Bi. Esther Mangenya na kufanya
mazungumzo ya namna bora ya kushirikiana katika kuboresha utoaji wa huduma za
afya msingi, elimu msingi na ujenzi wa miundombinu ya barabara pamoja
miundombinu ya huduma nyinginezo za kijamii.










No comments:
Post a Comment