Maisha ya mtaani yana tabia ya kukuponda mpaka unajiona huna thamani yoyote mbele ya jamii. Naitwa Hamisi, kijana ambaye nilitumia miaka saba ya ujana wangu nikihangaika kupata kazi bila mafanikio. Niliamua kugeukia michezo ya kubashiri (betting) kama njia ya kujikwamua, lakini badala ya neema, niliishia kuwa kituko cha mtaa.
Kila senti niliyopata kwa vibarua vya ujenzi, niliipeleka kuweka mikeka ambayo yote ilikuwa inachanika vibaya. Watu walianza kuniita “teja wa betting” na kila nilipopita, walikuwa wananicheka na kusema kuwa nimepoteza akili.
Hali ya kuonekana kituko iliniumiza sana moyoni, hasa ukizingatia umri wangu wa kuelekea miaka 35 ulikuwa unanidai kuanza kuwa na familia.








No comments:
Post a Comment