 |
Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Dodoma, Mengi Mwakisole, akizungumza na vijana wa umoja huo wa Kata ya Dodoma Makulu wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya leo Februari 21, 2026 Jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu wa UVCCM Kata ya Dodoma Makulu, Simon Yona na Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM wa Kata hiyo Dotto Chihoma ................................................. Na Dotto Mwaibale, Dodoma
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wametakiwa
kuwa mabalozi wa Amani nchini kutokana na umuhimu wao katika Taifa.
Wito huo umetolewa na Katibu wa umoja huo Wilaya ya Dodoma,
Mengi Mwakisole wakati akizungumza na mamia ya vijana wa Kata ya Dodoma Makulu
katika ziara yake ya kikazi iliyofanyika leo Februari 21, 2026 Jijini Dodoma.
“ Sisi Vijana kutokana na umuhimu wetu katika taifa ndiyo
tunaopaswa kuwa mabalozi wa kuhakikisha tuna itunza amani ya nchi yetu,” alisema
Mwakisole.
Mwakisole alisema watanzania hatuna nchi nyingine mbadala
ambayo tutaikimbia kwenda kuishi iwapo amani tuliyonayo tutaipoteza ambapo
alisisitiza umuhimu wa kuitunza kwa gharama yoyote ile.
Katika hatua nyingine Mwakisole amewaomba wanachama wa
jumuiya hiyo kuendelea kuwa na upendo, umoja na mshikamano baina yao, viongozi
na makundi mengine jambo litakalo saidia kuchagiza maendeleo ya nchi kwa kutekeleza
ilani ya CCM ya 2025/ 2030 chini ya Mwenyekiti wa Taifa wa
chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu
Hassan.
Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kukagua uhai wa jumuiya hiyo
ngazi ya matawi, kata, kusikiliza changamoto za vijana na kukumbushana juu
ya kutekeleza wajibu wa viongozi. Kabla ya kuzungumza na wanachama wa jumuiya hiyo kilifanyika kikao cha ndani na viongozi
mbalimbali wa ngazi ya matawi na Kata ya Dodoma Makulu kilichoongozwa na Katibu huyo wa UVCCM Wilaya
ya Dodoma, Mengi Mwakisole. Mwakisole kesho ataendelea na ziara yake hiyo Kata ya Ntyuka. Katibu wa UVCCM Kata ya Dodoma Makulu, Simon Yona, akizungumza wakati wa ziara hiyo. |
Viongozi meza kuu wakijadiliana
Kikao kikiendeleaWashiriki wa kikao hicho wakipitia masuala mbalimbali Kikao kikiendeleaUsikivu ukitamalaki kwenye kikao hicho.
Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale, simu namba 0754362990.
No comments:
Post a Comment