BALOZI CP KAGANDA AKUTANA NA MKURUGENZI WA IDARA YA AFRIKA NA ASIA KUIMARISHA USHIRIKIANO - SINGIDANI BLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, 13 March 2026

BALOZI CP KAGANDA AKUTANA NA MKURUGENZI WA IDARA YA AFRIKA NA ASIA KUIMARISHA USHIRIKIANO

Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Kamishna wa Polisi (CP) Suzan Kaganda, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika na Asia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Biashara za Kimataifa ya Zimbabwe, Bw. Mqabuko Dube.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika nchini Zimbabwe, viongozi hao walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zimbabwe, hususan katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na ushirikiano wa kikanda.

Aidha, pande zote mbili zilikubaliana kuendeleza na kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo mbili, pamoja na kushirikiana kwa karibu katika utekelezaji wa majukumu yao kwa lengo la kuchochea maendeleo ya pamoja na kuimarisha uhusiano wa kirafiki uliopo kati ya Tanzania na Zimbabwe.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad