Maisha ya kutafuta mafanikio kupitia michezo ya kubashiri ni safari yenye milima na mabonde, na wengi huishia kuumia mioyo yao kila kukicha. Mimi naitwa Amos, na kwa muda mrefu nilikuwa mmoja wa vijana waliokuwa wakipoteza kila senti waliyoipata kwenye vibanda vya betting.
Nilikuwa nafanya kazi ya kusukuma mkokoteni sokoni, na kila shilingi mbili niliyopata, niliipeleka kuweka mkeka nikiamini kuwa ipo siku Mungu ataniona. Lakini badala ya kuonwa, niliishia kudharaulika.
Marafiki zangu walinitenga na kuniona kama mtu aliyepoteza mwelekeo, huku mke wangu akinitishia kuniacha kwa sababu ya umaskini uliokithiri na njaa ndani ya nyumba.
Kila nilipoweka mkeka, hata kama nilikuwa nimechagua timu zenye uhakika wa asilimia mia moja, lazima timu moja ingeharibu mambo yote dakika za mwisho. Nilifikia hatua ya kuhisi kuwa labda kuna mkono wa mtu unanichezea, au labda nilizaliwa chini ya kivuli cha mikosi.

.jpg)






No comments:
Post a Comment