MTOTO WA MIAKA 12 AJINYONGA BAADA YA KUKEMEWA MOROGORO - SINGIDANI BLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Monday, 23 March 2026

MTOTO WA MIAKA 12 AJINYONGA BAADA YA KUKEMEWA MOROGORO

Mtoto mwenye umri wa miaka 12, Rajabu Ally Mohammed, mkazi wa Ijava wilayani Gairo mkoani Morogoro, amefariki dunia kwa kujinyonga baada ya kukemewa na wazazi wake kufuatia tuhuma za kujihusisha na vitendo vya udokozi.


Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Alex Mkama, amesema tukio hilo limegundulika  Machi 23, 2026 katika kitongoji cha Kaloleni, kata ya Italagwe, ambapo mtoto huyo alikutwa akiwa amejinyonga nyuma ya nyumba yao.

Kwa mujibu wa kamanda wa  Polisi uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Machi 22, 2026 mtoto huyo alikemewa na wazazi wake baada ya kukamatwa pamoja na wenzake wawili wakidaiwa kuiba mahindi mabichi.

 Inadaiwa kuwa kukemewa huko kulimfanya ajisikie vibaya na kuamua kujinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali yake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad