Meneja Miradi wa Shirika la Konrad Adenauer Tanzania, Damas Nderumaki akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya uandishi wa kidijitali yaliyoanza leo Machi 23, 2026 Hoteli ya Regency Mkoa wa Singida ambayo yatafikia tamati kesho.
....................................
Na Dotto Mwaibale, Singida
WAANDISHI wa Habari wa Kidijitali (Digital Journalism Training),wametakiwa kujenga mahusiano ili kupata fursa zinazopatikana kwenye mitandao mbalimbali ya Kijamii.
Hayo yamebainishwa na Meneja Miradi wa Shirika la Konrad Adenauer Tanzania, Damas Nderumaki wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya uandishi wa kidijitali yaliyofanyika Mkoa wa Singida Hoteli ya Regency.
“Nasisitiza jambo hili la Networking kwa sababu mimi ni mnufaika na bila ya mitandao hii nisingeweza kukutana na ninyi hapa leo,” alisema Nderumaki.
Aidha, Nderumaki aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kumuona kila mtu kuwa ni fursa ya kusonga mbele katika shughuli zao za kila siku.
Mtendaji Mkuu wa Media Brains, Jesse Kwayu alisema waandishi wa habari wa kidijitali wanapaswa kuzingatia misingi na maadili yote ya kiuandishi kama ilivyo kwa vyombo vingine vya habari.
“Uandishi wa habari za kidijitali ni sawa na vyombo vingine vya habari hivyo inatakiwa kufuata misingi na sheria za kiuandishi,” alisema Kwayu.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Media Brains, Absalom Kibanda alisema habari zinazotengenezwa zitatakiwa kuwa sahihi na kuzisambaza kwa kuwashirikisha wapokeaji wa habari hizo.
Mafunzo hayo ambayo ni mahususi kuwajengea uwezo waandishi wa kidijitali Mkoa wa Singida yameandaliwa na Kampuni ya Media Brains (Brain Incorporated Ltd) ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Taasisi ya Konrad Adenauer Stiftung (KAS) ya Ujerumani Ofisi ya Tanzania,
Mtendaji Mkuu wa Media Brains, Jesse Kwayu, akitoa mada kwenye mafunzo hayo.Mkuu wa Uendeshaji wa Media Brains, Absalom Kibanda, akisisitiza jambo wakati akitoa mada kwenye mafunzo hayo.
Mratibu wa Mafunzo wa Media Brains, Neville Meena akisisitiza jambo kwenye mafunzo hayo.
Taswira ya mafunzo hayo.
Wanahabari wa kidijitali Mkoa wa Singida wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea. Kutoka kushoto ni mwanahabari Thobias Mwanakatwe, Elisante Mkumbo na Michael Ramadhani.
Wanahabari Emmanuel Michael na Abby Nkungu (kulia) wakionesha furaha zao wakati wa mafunzo hayo.







No comments:
Post a Comment