Aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Vangimembe Lukuvi amefariki hii leo Machi 25, 2026, majira ya saa moja asubuhi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Jijini DodomaTaarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka imeeleza kuwa Lukuvi amekubwa na umauti katika Hospitali hiyo, alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mshtuko wa moyo.
Kufuatia msiba huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa Spika wa Bunge, familia, Wananchi wa Jimbo la Isimani, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huo.








No comments:
Post a Comment