..............................
Na Dotto Mwaibale,
JUMUIYA ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma kesho kufanya maadhimisho ya wiki ya Wazazi 2026 kwa kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kufanya usafi.
Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 8, 2026 Katibu wa
Jumuiya hiyo Wilaya ya Kibondo, Evarist Mwonone alisema maandalizi yote ya
maadhimisho hayo yamekwisha kamilika.
“Maandalizi yote ya maadhimisho hayo yamekwisha kamilika pamoja na wageni waalikwa kuthibitisha kuhudhuria ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo Hamisi Salum Tahiro,” alisema Mwonone.
Alisema maadhimisho hayo kiwilaya yatafanyika kesho Aprili
9, 2026 katika Kata ya Kizazi Tarafa ya Mabamba.
Katibu huyo wa jumuiya hiyo wilayaaani humo alisema
maadhimisho hayo yatafanyika sambamba na shughuli za kijamii kama kufanya usafi
maeneo ya Kituo cha Afya cha kata hiyo pamoja na kutoa misaada kwa makundi mbalimbali ya watu wenye uhitaji
wakiwemo wazee.
Alisema tukio hilo la utoaaji wa misaada hiyo litafanyika
kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika katika kata hiyo ambapo alitumia nafasi
hiyo kuwaalika wananchi wote kwenda kushiriki.
Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale namba ya simu 0754362990








No comments:
Post a Comment