MTATIFIKOLO ACHUKUA FOMU KUWANIA NAFASI YA UBUNGE ISIMANI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, April 19, 2026

MTATIFIKOLO ACHUKUA FOMU KUWANIA NAFASI YA UBUNGE ISIMANI

Emmanuela Mtatifikolo, ameonesha dhamira yake ya dhati ya kuwatumikia wananchi kwa kuchukua na kurejesha fomu ya kuwania nafasi ya ubunge katika Jimbo la Isimani.

Hatua hii inaakisi utayari wake wa kupeleka uzoefu wake mpana wa kiuongozi katika ngazi ya juu ya uwakilishi wa wananchi.

Akiwa ni kiongozi mahiri mwenye rekodi ya utendaji uliotukuka, Emmanuela amewahi kushika nafasi mbalimbali muhimu serikalini na katika taasisi za kitaifa na kimataifa.

Kwa sasa anahudumu kama Mkuu wa Wilaya ya Babati (2024 – sasa), baada ya kuitumikia nchi kama Mkuu wa Wilaya ya Arumeru (2023 – 2024). Kabla ya hapo, alikuwa Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Jitegemee Holdings Co. Ltd (2021 – 2024), akionesha ubunifu na umahiri katika kuendesha miradi ya maendeleo. Aidha, aliwahi kuwa Mratibu wa Mradi katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (Kibaha), Afisa Mchambuzi wa Miradi katika UNFPA 2016 – 2017, pamoja na Programme Officer for Africa katika taasisi ya UEM, akiratibu miradi katika nchi mbalimbali za Afrika na Asia.

Kitaaluma, Emmanuela ana sifa madhubuti zinazomuimarisha katika uongozi na utumishi wa umma. Ana Shahada ya Uzamili ya Afya ya Jamii Master of Public Health kutoka Chuo Kikuu cha Jiji la New York (2014 – 2017), pamoja na Stashahada ya Afya ya Jamii kutoka chuo hicho hicho. Vilevile, ana Shahada ya Sanaa katika Mawasiliano ya Umma (Mass Communication) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Mwanza (2001 – 2004).

Mchanganyiko huu wa elimu na uzoefu unamfanya kuwa kiongozi mwenye maono, uthubutu, na uwezo wa kuleta mageuzi chanya kwa wananchi wa Isimani.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad