Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Mtatifikolo, amesema kuwa taasisi za kidini zina nafasi kubwa katika kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania na wananchi wengine wanaoishi nchini huku akiomba wananchi na viongozi wa dini na serikali kupambana ma adui mmomonyoko wa maadili.
Rai hiyo aliitoa Aprili 16, 2026, wakati wa uzinduzi wa Parokia Teule ya Mtakatifu Anna Mrara ambapo Uzinduzi huo ulifanywa na Askofu wa Jimbo la Mbulu, Askofu Antony Lagwen, akishirikiana na Askofu wa Jimbo la Bunda na Geita.
Aidha, Mhe. Mtatifikolo alisisitiza kuwa amani na utulivu ni misingi muhimu inayopaswa kuendelezwa na viongozi wa dini serikali ma wananchi kwa ujumla ambapo aliongeza kuwa jamii inakabiliwa na changamoto ya mmomonyoko wa maadili, hivyo akatoa wito kwa viongozi wa dini kushirikiana na serikali katika kukemea vikali hali hiyo ili kulinusuru taifa dhidi ya janga hilo linalokua kwa kasi.
Vilevile, alibainisha kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa Rais Dr Samia Suluhu Hassan, itaendelea kushirikiana na taasisi zote za kidini pamoja na viongozi wake katika kulinda na kudumisha amani na utulivu uliopo nchini kwa muda mrefu.
Sambamba na hayo akawaomba viomgozi hao wa dini wakiongozwa na Baba askofu wa Jimbo la Mbulu kuiombea Serikali ili viongozi wake waendelee kuwahudumia vyema wananchi.










No comments:
Post a Comment