Kwa muda fulani nilianza kugundua vitu vidogo vidogo vikipotea nyumbani kwangu. Kwanza ilikuwa pesa ndogo mezani, kisha vitu vya jikoni, na baadaye hata baadhi ya vifaa vya thamani ndogo ndogo. Mwanzoni nilidhani ni mimi ninasahau au kuweka vibaya, lakini hali ilipoendelea nikajua kuna mtu anaeingia bila ruhusa.
Kilichoniumiza zaidi ni kwamba haikuwa rahisi kujua nani alikuwa nyuma ya yote hayo. Nyumba yangu haikuwa na dalili za uvunjaji, na watu wachache tu ndio waliokuwa wakija. Nilianza kuwa na wasiwasi hata kwa watu wa karibu, jambo lililonifanya nihisi sintofahamu ndani ya nyumba yangu mwenyewe.








No comments:
Post a Comment