Maumivu yalianza kama kitu kidogo tu. Tumbo lilikuwa linaniuma mara kwa mara, hasa usiku na asubuhi. Mwanzoni nilipuuzia, nikidhani ni chakula au uchovu. Lakini kadri siku zilivyopita, maumivu yalizidi kuwa makali na ya mara kwa mara.
Nilienda hospitali mara kadhaa. Nilifanyiwa vipimo tofauti damu, mkojo, hata scan. Kila mara niliambiwa hakuna tatizo kubwa limeonekana. Nilipatiwa dawa za kupunguza maumivu, lakini hazikudumu. Baada ya muda mfupi, hali ilirudi vile vile.








No comments:
Post a Comment