Wachezaji wa Mpira wa Pete (Netball) ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika picha ya pamoja wakati walipokuwa wanajiandaa kufanya mazoezi ya pamoja Aprili 15, 2026 kuelekea mashindano ya Mei Mosi ikiwa ni shamrashamra ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2026

Kocha wa Mpira wa Pete (Netball) ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Mafuru Buriro akifanya mazoezi na mmoja wa wachezaji wa timu hiyo Aprili 15, 2026 kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya michezo ya mei mosi ikiwa ni shamrashamra ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2026 yanayotarajia kufanyika Kitaifa Mkoani Njombe.
Wachezaji wa Mpira wa Pete (Netball) ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakifanya ya pamoja ya timu hiyo Aprili 15, 2026 kujiandaa na mashindano ya Mei Mosi ikiwa ni shamrashamra ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2026 yanayotarajia kufanyika Kitaifa Mkoani Njombe.
Wachezaji wa Mpira wa Pete (Netball) ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakifanya mazoezi ya pamoja ya timu hiyo Aprili 15, 2026 kujiandaa na mashindano ya Mei Mosi ikiwa ni shamrashamra ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2026 yanayotarajia kufanyika Kitaifa Mkoani Njombe.

Wachezaji wa Mpira wa Pete (Netball) ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakiomba dua ya pamoja Aprili 15, 2026 wakati wa mazoezi ya timu hiyo kujiandaa na mashindano ya Mei Mosi ikiwa ni shamrashamra ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2026 yanayotarajia kufanyika Kitaifa Mkoani Njombe.
Wachezaji wa Mpira wa Pete (Netball) ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakifanya mazoezi ya pamoja Aprili 15, 2026 kujiandaa na mashindano ya Mei Mosi ikiwa ni shamrashamra ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2026 yanayotarajia kufanyika Kitaifa Mkoani Njombe.
Kocha wa Mpira wa Pete (Netball) ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Mafuru Buriro akifuatalia mazoezi ya wachezaji wa timu hiyo inayoajindaa na mashindano ya Mei Mosi ikiwa ni shamrashamra ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2026 yanayotarajia kufanyika Kitaifa Mkoani Njombe.
Wachezaji wa Mpira wa Pete (Netball) ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakifanya mazoezi ya pamoja Aprili 15, 2026 kujiandaa na mashindano ya Mei Mosi ikiwa ni shamrashamra ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2026 yanayotarajia kufanyika Kitaifa Mkoani Njombe.
Wachezaji wa Mpira wa Pete (Netball) ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakifanya mazoezi ya pamoja Aprili 15, 2026 kujiandaa na mashindano ya Mei Mosi ikiwa ni shamrashamra ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2026 yanayotarajia kufanyika Kitaifa Mkoani Njombe.
Baadhi ya Wachezaji wa Mpira wa Pete (Netball) ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakifuatilia mazoezi ya pamoja Aprili 15, 2026 wakati wa maandalizi na mashindano ya Mei Mosi ikiwa ni shamrashamra ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2026 yanayotarajia kufanyika Kitaifa Mkoani Njombe.
-----------------------------------
Na Mwandishi Wetu- Njombe
Timu ya Mpira wa Pete (Netball) ya Ofisi ya Makamu wa Rais inatarajia kufungua pazia la Michezo ya Mei Mosi, 2026 kwa kuumana na Timu ya Wizara ya Maji tarehe Aprili 16 mwaka huu.
Ratiba iliyotolewa Aprili 15, 2026 na Kamati ya Mashindano ya Mei Mosi Taifa, 2026 imesema mchezo huo unatarajia kufanyika katika Uwanja wa Mji Mwema, Njombe ukiwa ni sehemu ya shamrashamra ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambayo kitaifa yanafanyika Mkoani humo.
Akizungumza kuhusu mchezo wa ufunguzi, Katibu wa Klabu ya Michezo Ofisi ya Makamu wa Rais, Marwa Nyaisawa amesema timu hiyo imejiandaa vyema kutoa ushindani kwa timu zote itakazokabiliana nazo katika michezo hiyo.
“Tunatambua ni mara yetu ya kwanza kushiriki michezo hii kupitia timu ya mpira wa pete lakini kwa maandalizi tuliyofanya tunatarajia kutoa ushindani kwa timu zote kuanzia hatua ya makundi hadi kuendelea” amesema Nyaisawa.
Ameongeza kuwa timu hiyo inatambua ugumu wa michezo ya Mei Mosi,2026 kwa wapinzani wanaoshiriki mashindano hayo kwani kila timu imejiandaa vyema, hata hivyo benchi la ufundi la timu hiyo limeweza kujenga morali na hali ya kujiamini kwa wachezaji wa kikosi chao.
Amesema ratiba ya michezo hiyo imepangwa vizuri ambapo katika hatua ya makundi, Timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais imepangwa Kundi H ikiwa na Timu nyingine ambazo ni Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Ameeleza kuwa mara baada ya mchezo na Wizara ya Maji, Timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais itacheza mchezo wa pili tarehe 17 Aprili, 2026 dhidi ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kabla ya kuhitimisha mechi ya mwisho ya hatua ya makundi dhidi ya Timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki tarehe 18 Aprili, 2026.
Kwa upande wake, Kocha wa Timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Mafuru Buriro amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya michezo hiyo ambayo wataitumia kwa ajili ya kusuka kikosi imara kinachotarajia kutoa ushindani katika mashindano mbalimbali ya kitaifa ya mpira wa pete.
“Wachezaji wote wapo tayari na tunazidi kuimarika siku hadi siku na benchi la ufundi linafanyia kazi kasoro ndogo ndogo tunaziona katika uwanja wa mazoezi na tumekusudia kuonesha kitu tofauti kwa wapinzani wetu katika michezo hii” amesema Buriro.
Kauli mbiu ya Michezo ya Mei Mosi, 2026 inasema “Michezo kwa Afya, Ajira, Furaha na Kazi Inaendelea; Kazi zenye staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira 2050”

No comments:
Post a Comment