𝐑𝐂 𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈𝐃𝐀 𝐀𝐏𝐎𝐍𝐆𝐄𝐙𝐀 𝐌𝐀𝐏𝐈𝐍𝐃𝐔𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐔𝐓𝐄𝐍𝐃𝐀𝐉𝐈 𝐓𝐀𝐍𝐄𝐒𝐂𝐎 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, April 30, 2026

𝐑𝐂 𝐒𝐈𝐍𝐆𝐈𝐃𝐀 𝐀𝐏𝐎𝐍𝐆𝐄𝐙𝐀 𝐌𝐀𝐏𝐈𝐍𝐃𝐔𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐔𝐓𝐄𝐍𝐃𝐀𝐉𝐈 𝐓𝐀𝐍𝐄𝐒𝐂𝐎

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego (katikati), Aprili 30, 2026, akikata utepe kuashiria kukabidhi vyombo vya usafiri kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani humo vilivyotolewa na Serikali. Wengine ni viongozi wa shirika hilo Mkoa wa Singida.
..........................

MKUU wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego amepongeza mapinduzi na mageuzi makubwa ya kiutendaji yanayofanywa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), hususani mkoani humo.


Mhe. Dendegu ametoa pongezi hizo Aprili 30, 2026 wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vyombo vya usafiri (Magari Manne) ya shirika hilo Mkoa wa Singida yaliyotolewa na Serikali kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa kazi.


“Awali ya yote nichukue nafasi hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali anayoingoza kwa jitihada kubwa anayoifanya ya kuwajengea uwezo watumishi, kuwapeleka shule. kuongeza wafanyakazi wapya na kuwaletea vitendea kazi, huu ni uwekezaji mkubwa unaofanywa ili muweze kufanya kazi vizuri,” alisema Dendego.


Aidha, alipongeza Tanesco Singida kwa kazi kubwa wanayoifanya chini ya Meneja wa shirika hilo mkoani humo, Mhandisi Mwamvita Ally na timu yake na kueleza kuwa tangia afike Singida hajawahi kuona changamoto kubwa ya umeme isipokuwa ile ya kijumla.


Alisema changamoto siku zote zipo, akitolea mfano mvua zinaponyesha nguzo zinaanguka na nyingine nyingi lakini anafurahi anapoona zinapotokea wanapata taarifa na hatua za kuzitatua zinapofanyika kwa wakati.


“Ikitokea hitilafu tu mnatuambia na mnaifanyia kazi kwa wakati haya ni mapinduzi na mageuzi makubwa ya kiutendaji ndani ya Tanesco chini ya Mkurugenzi Mtendaji Lazaro Twange,” alisema Dendego.


Aliongeza kuwa hivi sasa umeme siyo anasa ni uchumi na ndiyo kila kitu hivyo tunapotekeleza dira ya Taifa ya 20 / 50 malengo yetu yatafikiwa kwa nyinyi kuhakikisha tunapata huduma ya umeme wa kutosha ambapo pia alihimiza magari hayo yatunzwe.


Kwa upande wake Meneja wa shirika hilo Mkoa wa Singida, Mhandisi Mwamvita Ally aliishukuru Serikali chini ya Rais Samia kwa kuwapatia magari hayo ambapo aliahidi kuyaatunza na kuhakikisha yatatumika kwa ajili ya kuwahudumia wananchi.


Afisa Usalama wa shirika hilo Mkoa wa Singida, Emilini Ndahani aliishukuru Serikali kwa kuwapa magari hayo na kueleza kuwa watahakikisha yanatumika kwa kazi iliyokusudiwa.


“Tunamshukuru sana mkurugenzi wetu Lazaro Twange kwa jitihada alizofanya na kutupatia magari haya ambayo yanakwenda kutoa huduma kwa wananchi na tutazingatia usalama wake pamoja na watu kwa kuwaelekeza madereva matumizi bora ya magari hayo,” alisema Ndahani.


Naye Mhandisi Boniface Shitindi wa shirika hilo Mkoa wa Singida alimshukuru Rais Samia kwa kuwashika mkono na kuweza kutoa magari hayo ambayo yanakwenda kuwapa tija ya kikazi.


“ Jambo ili kwetu ni chachu ya kuongeza uchumi wa Taifa letu kama kauli mbiu yetu inavyo sema “Tunayaangaza Maisha” ndivyo tunavyoendelea kuyaangaza kupitia magari hayo tuliyopatiwa na Serikali.


Vyombo vya usafiri vilivyo kabidhiwa ni Land Cruiser mbili mpya na mashine mbili za kuinua vitu vizito zikiwemo nguzo.Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, akizungumza kwenye hafla hiyo.Meneja wa shirika hilo Mkoa wa Singida, Mhandisi Mwamvita Ally akizungumza.Afisa Usalama wa shirika hilo Mkoa wa Singida, Emilini Ndahani, akizungumza.Mhandisi Boniface Shitindi wa shirika hilo Mkoa wa Singida, akizungumza.Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego (katikati), akiwa na viongozi wa shirika hilo wakati wa hafla hiyo.Vyombo vya usafiri vilivyokabidhiwa.

Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale namba ya simu 0754362990.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad