Meneja Mkuu wa Taifa Gas, Devis Deogratius.
Taifa Gas haitapandisha
bei ya gesi ya majumbani (LPG) licha ya ongezeko la takribani asilimia 43 ya bei
ya gesi hiyo duniani. Hatua hii ni sehemu ya juhudi za kampuni hiyo kuendeleza
upatikanaji nafuu wa nishati hiyo pamoja
na kupunguza za athari za mabadiliko ya soko la kimataifa kwa wateja wake.
Katika taarifa yake
kwa vyombo vya habari, Taifa Gas imeeleza kuwa soko la kimataifa la gesi ya
kupikia limekumbwa na ongezeko kubwa la
bei katika wiki za hivi karibuni
na hivyo kusababisha kuongezeka kwa gharama za ununuzi katika minyororo ya
ugavi na usambazaji duniani.
“Katika mazingira haya
ya sasa, tunayo dhamira ya dhati ya kuwasaidia wateja wetu kwa kubeba athari za
ongezeko la gharama ya nishati ya kupikia kwa kutokuongeza bei huku
tukihakikisha upatikanaji endelevu wa gesi safi na ya kuaminika,” alisema Meneja
Mkuu wa Taifa Gas, Devis Deogratius.
Nishati Nafuu na Utulivu
wa Kiuchumi
Taifa Gas imesema
kuwa kipaumbele chake kwa sasa ni kuhakikisha bei hiyo ya nishati haiongezeki hivyo, kutoa mchango muhimu kwenye shughuli za
kiuchumi huku ikitambua kuwa gesi ya kupikia
ni nishati muhimu katika kaya na biashara ndogo ndogo nchini Tanzania.
Deogratius alisema, “Tunatambua
kuwa gesi ya kupikia ni nishati muhimu kwa Watanzania wengi na lengo letu ni
kuhakikisha kwamba inapatikana kwa bei
nafuu huku tukidumisha usambazaji
wa uhakika kote nchini.”
Upatikanaji na Usambazaji wa Gesi Nchini
Taifa Gas inauthibitishia
umma kwamba usambazaji wa bidhaa zake utaendelea
kuwa thabiti kupitia mtandao wake wa maghala 25 yaliyopo nchini kote
hivyo, kuhakikisha upatikanaji wa gesi ya kupikia katika maeneo ya mijini na
vijijini.
“Tanzania ni nchi
kubwa na yenye mahitaji tofauti hivyo upatikanaji wa nishati hii ni kipaumbele
kikubwa kwetu sisi,” alisema Deogratius na
kuongeza kwamba, “tumewekeza
katika miundombinu inayotuwezesha kusambaza gesi ya kupikia sehemu mbalimbali
nchini.”
Nishati Safi na Vipaumbele vya Kitaifa
Taifa Gas imeeleza
kuwa inaendelea kuzingatia vipaumbele vya kitaifa vya nishati pamoja na Malengo
ya Maendeleo Endelevu (SDGs), hasa katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi
ya kupikia na hivyo, kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.
Kampuni hiyo imeeleza
kwamba upatikanaji wa LPG unachangia
kuboresha afya za wananchi, kulinda mazingira, na kuchangia katika
ushirikishwaji wa wananchi kwenye Uchumi
wa nchi.
Dhamira Endelevu
Taifa Gas
imesisitiza kuwa itaendelea kuufuatilia mwenendo wa soko la kimataifa huku
ikiendelea kufanya kazi ndani ya mifumo ya sekta ya nishati ili kuwasaidia
wateja kwa kudumisha utulivu wa bei kadri itavyowezekana.
“Jukumu letu ni kuwauunga
mkono na
kuwalinda Watanzania kwa kuwapa huduma bora, kuwa na uendeshaji wenye
uwajibikaji, na dhamira ya muda mrefu ya kuhakikisha upatikanaji wa nishati
safi nchini,” alisema Deogratius.
Kuhusu Taifa Gas
Taifa Gas ni kampuni
ya nishati ya Tanzania inayojihusisha na usambazaji wa gesi ya majumbani (LPG.) Kampuni hii inaendesha kituo kikubwa
zaidi cha kuhifadhi LPG nchini na ina mtandao mpana zaidi wa usambazaji wenye
maghala 25 nchini kote. Kampuni hii imejikita
katika kupanua upatikanaji wa nishati safi, nafuu na ya kuaminika.








No comments:
Post a Comment