TMDA YATOA ELIMU JUU YA UTOAJI TAARIFA ZA MADHARA NA MATUKIO YA VIFAA TIBA NA VITENDANISHI NA UZINGATIAJI WA MATUMIZI SAHIHI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, April 12, 2026

TMDA YATOA ELIMU JUU YA UTOAJI TAARIFA ZA MADHARA NA MATUKIO YA VIFAA TIBA NA VITENDANISHI NA UZINGATIAJI WA MATUMIZI SAHIHI

Kaimu Meneja Ufatiliaji Usalama wa Vifaa Tiba na Vitendanishi TMDA, Davidi Matle  akizungumza wakati wa  mafunzo kwa Wataalam wa Afya katika vituo vya kutolea huduma (Hospitali, Vituo vya Afya, Zahanati ) kuhusu matumizi ya vifaa tiba  vitendanishi na uzingatiaji wa matumizi sahihi.
-----------------------------------------------------
Afisa Ufuatiliaji wa Ubora, Usalama na Ufuatiliaji kutoka TMDA Makao Makuu Dkt. Nassoro Matuzya akizungumza wakati wa  mafunzo kwa Wataalam wa Afya katika vituo vya kutolea huduma.
Muhandisi TMDA Kanda ya Kati. Einoth Nicholas akitoa mada wakati wa mafunzo hayo.
Watoa huduma za afya wakiwa katika mafunzo.
Kaimu Mganga Mfawidhi Hospital ya Wilaya ya Ikungi, Milali Kezilahabi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mafunzo hayo.
Mganga Mfawidhi kituo cha Afya ya  Ikungi, Reward Emmanuel akizungumza.
Mratibu wa Vifaa Tiba Ikungi,Elfrida Deogratias akizungumza.
Kaimu Mganga Mfawidhi Zahanati ya Ighuka,Raukhiya Sikuni akizungumza.
Mafunzo yakiendelea.
-----------------------------------------

Wataalam wa Afya katika vituo vya kutolea huduma (Hospitali, Vituo vya Afya, Zahanati n.k) wamehimizwa kuzingatia matumizi sahihi ya vifaa tiba na vitendanishi ili kupunguza malalamiko, madhara na matukio hasi. Ushauri huo umetolewa na Ndg. David Robert Matle - Kaimu Meneja Ufuatiliaji wa Ubora, Ufanisi na Usalama wa vifaa tiba na vitendanishi kutoka TMDA makao makuu Dodoma wakati akitoa mafunzo kwa watoa huduma hao yaliyofanyika katika vituo 9 mbalimbali katika Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida kuanzia Aprili 08 hadi 10, 2026 kwa nyakati tofauti.


Bw. Matle, amesema ya kuwa matumizi yasiyo sahihi yanaweza kusababisha madhara makubwa yakiwemo malalamiko na matukio yatokanayo na matokeo yasiyo sahihi ya uchunguzi na hata kuhatarisha maisha ya wanufaika (Mgonjwa).


"Vifaa tiba kama vile sindano, mashine mbalimbali za kupimia pamoja na vitendanishi vinavyotumika vinapaswa kutumika kulingana na miongozo iliyowekwa na watengenezaji" alisisitiza. Dkt. Nassoro Ally Matuzya 


- Afisa Ufuatiliaji wa Ubora, Usalama na Ufuatiliaji kutoka TMDA Makao Makuu pia amesema matumizi sahihi ya vifaa tiba na vitendanishi si tu kwamba yanaongeza ubora wa huduma, bali pia yanaimarisha imani kwa jamii kwa watendaji katika sekta ya Afya nchini katika utekelezaji wa sera ya Afya kwa jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad