Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha, wakiwa katika maandamano ya Mei Mosi wakielekea katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya kushiriki Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani 2026 yanayofanyika kimkoa jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha, wakiwasili katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kwa ajili ya kushiriki Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), ngazi ya mkoa.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha, wameshiriki sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), ambapo kwa ngazi ya Mkoa wa Dodoma yamefanyika katika Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.
Maadhimisho ya Siku hii ya Wafanyakazi Duniani kitaifa, yamefanyika katika Mkoa wa Njombe ambapo pia baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha wameshiriki sherehe hizo.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani nchini, kwa mwaka huu ni ‘’Kazi Zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo Endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050’’.
Maadhimisho haya hufanyika kila ifikapo tarehe moja mwezi Mei kila mwaka ambapo wafanyakazi wa Serikali na Sekta binafsi huwasilisha changamoto zao mbalimbali ikiwemo mazingira bora ya kazi, maombi ya nyongeza ya mishahara, malipo ya likizo pamoja na mambo mengine muhimu yanayoweza kuongeza morali yao ya kazi pamoja na tija kwa Taifa.

No comments:
Post a Comment