𝐃𝐊𝐓 𝐀𝐊𝐖𝐈𝐋𝐀𝐏𝐎 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐃𝐀𝐈𝐖𝐀 𝐖𝐀 𝐊𝐎𝐃𝐈 𝐘𝐀 𝐏𝐀𝐍𝐆𝐎 𝐋𝐀 𝐀𝐑𝐃𝐇𝐈 𝐊𝐈𝐆𝐎𝐌𝐀 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, May 1, 2026

𝐃𝐊𝐓 𝐀𝐊𝐖𝐈𝐋𝐀𝐏𝐎 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐃𝐀𝐈𝐖𝐀 𝐖𝐀 𝐊𝐎𝐃𝐈 𝐘𝐀 𝐏𝐀𝐍𝐆𝐎 𝐋𝐀 𝐀𝐑𝐃𝐇𝐈 𝐊𝐈𝐆𝐎𝐌𝐀

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe, Simon Siro (Kushoto) wakati wa kikao cha Waziri wa Ardhi na Wadaiwa Sugu wa Kodi ya Pango la Ardhi mkoa wa Kigoma tarehe 30 April 2026.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akizungumza na wadaiwa Sugu wa Kodi ya Pango la Ardhi mkoa wa Kigoma tarehe 30 April 2026.
Sehemu ya washiriki wa kikao cha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi mkoa wa Kigoma tarehe 30 April 2026.
Mkuu wa wilaya ya Kigoma Dkt Rashid Chuachua akizungumza wakati wa wa kikao cha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Akwilapo na Wadaiwa Sugu wa Kodi ya Pango la Ardhi mkoa wa Kigoma tarehe 30 April 2026.
Washiriki wa kikao cha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo na wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi mkoa wa Kigoma tarehe 30 April 2026.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo (katikati) pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kigoma Dkt, Rashid Chuachua (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wadaiwa wa Kodi ya Pango la Ardhi mkoa wa Kigoma tarehe 30 April 2026.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo (Kulia), Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe, Simon Siro (Katikati) na Kaimu Kamishna wa Ardhi Msaidzi mkoa wa Kigoma Bw. Tumaini Gwakisa wakiwa katika kikao cha Wadaiwa Sugu wa Kodi ya Pango la Ardhi mkoa wa Kigoma tarehe 30 April 2026. 
-------------------------------

#Asisitiza umuhimu wa kulipa Kodi ya ardhi kwa wakati

 

#Aahidi kushughulikia changamoto zinazowakabili

 

Na Munir Shemweta, KIGOMA

 

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo amekutana na kumfanya mazungumzo na wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Kigoma zikiwemo taasisi za umma na binafsi. Kiasi cha shilingi Bilioni 6.2 kinadaiwa kwa taasisi hizo na watu binafsi mkoani humo. 

 

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika tarehe 30 April, 2026 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa Kigoma, Mhe. Dkt Akwilapo amesema kati ya kiasi hicho cha fedha taasisi za umma pekee zinadaiwa shilingi Bilioni 5.8, taasisi binafsi milioni 272.4 na watu binafsi miliomi 116.4.

 

‘’Kila mtu anayemiliki kipande cha ardhi ana haki na wajibu wa kulipa kodi ya pango la ardhi Kwa mujibu wa Sheria ya ardhi Namba 4 ya Mwaka 1999’’. Amesema Dkt Akwilapo

 

Amewaelekeza makamisha wa Ardhi Wasaidizi wa Mikoa kuanza kuchukua hatua kwa wadaiwa ambao hawajatekeleza wajibu wao wa kisheria wa kulipa Kodi ya ardhi kwa kutii Sheria.

 

"Niwakumbushe wote wasiolipa kodi ya pango la ardhi hata kama hawajatumiwa ankara za Kodi wafike Ofisi za Ardhi za Mikoa ili waelezwe na kupewa ankara kuepuka malimbikizo ya madeni,riba pamoja na kuchukuliwa hatua za kisheria.

 

Waziri huyo wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewataka wamiliki wa ardhi waliobadilisha Namba za simu kwenda Ofisi za Ardhi kuhuisha namba zao za simu ili waweze kupata Ankara za bili zao kupitia jumbe za simu za mkononi.

 

Katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za sekta ya ardhi kwa haraka, Mhe. Dkt Akwilapo amewataka wananchi kufika katika Kliniki za ardhi zinazoendeshwa maeneo mbalimbali nchini ili waweze kuhudumiwa.

 

Awali taasisi za umma na binafsi kupitia wawakilishi wao walimueleza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi baadhi ya changamoto wanazopata wakati wa kutekeleza wajibu wao wa kulipa kodi ambapo wametaja moja ya changamoto hizo ni kukadiriwa kodi kwa eneo kubwa tofauti na uhalisia wa eneo husika wanalomiliki.

 

" Tunaenda kulipa kitu ambacho hatukitumii, eneo letu ni square mita 1,129 lakini wewe Ofisi unatuambiwa tunadaiwa square mita 5,000 ni haki kwelii? Amesema mmoja wa wadaiwa sugu.

 

Dkt Akwilapo aliziahidi taasisi hizo za umma, binafsi pamoja na wananchi wengine kuwa changamoto walizowasilsha kwake zitafanyiwa kazi ndani ya muda mchache na kuomba ushirikiano wakati wote wa kushughulikia changamoto hizo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad