𝐑𝐀𝐈𝐒 . 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐍𝐘𝐎𝐓𝐀 𝐖𝐀 𝐙𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐖𝐀 𝐓𝐈𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐘𝐀 𝐈𝐕𝐎𝐑𝐘 𝐂𝐎𝐀𝐒𝐓 𝐍𝐀 𝐓𝐈𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐂𝐇𝐄𝐋𝐒𝐄𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐈𝐍𝐆𝐄𝐑𝐄𝐙𝐀 𝐃𝐈𝐃𝐈𝐄𝐑 𝐃𝐑𝐎𝐆𝐁𝐀 - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Tuesday, May 5, 2026

𝐑𝐀𝐈𝐒 . 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐍𝐘𝐎𝐓𝐀 𝐖𝐀 𝐙𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐖𝐀 𝐓𝐈𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐘𝐀 𝐈𝐕𝐎𝐑𝐘 𝐂𝐎𝐀𝐒𝐓 𝐍𝐀 𝐓𝐈𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝐂𝐇𝐄𝐋𝐒𝐄𝐀 𝐘𝐀 𝐔𝐈𝐍𝐆𝐄𝐑𝐄𝐙𝐀 𝐃𝐈𝐃𝐈𝐄𝐑 𝐃𝐑𝐎𝐆𝐁𝐀

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mshambuliaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast na Timu ya Chelsea ya Uingereza Didier Drogba mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 05 Mei, 2026.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mshambuliaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast na Timu ya Chelsea ya Uingereza Didier Drogba mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 05 Mei, 2026. Katika mazungumzo yao Mhe. Rais Dkt. Samia amemuomba Nyota huyo Ivory Coast kuwa Balozi wa Tanzania kuelekea Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027. Aidha, Rais Dkt. Samia ameitaka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kushirikiana na mchezaji huyo kubadilishana uzoefu wa kuendesha Vituo vya michezo nchini (Sports Academy). Mchezaji huyo amemshukuru Rais Dkt. Samia na kuonesha utayari wa kushirikiana na Serikali. Pamoja na mafanikio kadhaa aliyoyapata katika Mpira wa miguu, Mwaka 2005, alifanya ushawishi uliosaidia kusitishwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini kwao vilivyodumu kwa miaka kadhaa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mshambuliaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast na Timu ya Chelsea ya Uingereza Didier Drogba, Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, tarehe 05 Mei, 2026.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad