Kwa miaka mingi nilifanya kazi sehemu moja huku nikihisi kama sionekani kabisa. Nilikuwa nafika mapema kazini, nafanya kazi zangu kwa bidii, na mara nyingi hata kusaidia wengine walipokwama.
Lakini cha kushangaza, juhudi zangu hazikuonekana kuwa na maana mbele ya watu wengi. Wafanyakazi wenzangu walikuwa wananicheka kwa siri.
Kila nilipotoa wazo kwenye mikutano, kulikuwa na watu waliolipuuzia au hata kulifanya mzaha.
Wakati mwingine nilikuwa naambiwa maneno ya kuniumiza kana kwamba sikuwa na uwezo wowote. Kilichoniumiza zaidi ni namna bosi wangu alivyonichukulia.









No comments:
Post a Comment