ASIA HALAMGA FOUNDATION YAKABIDHI MAJIKO YA GESI KUSAIDIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO HANANG' - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, 23 December 2023

ASIA HALAMGA FOUNDATION YAKABIDHI MAJIKO YA GESI KUSAIDIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO HANANG'

Mbunge wa Vijana Taifa, Asia Halamga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  wakati akitoa msaada wa majiko ya gesi 50 kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa maporomoko ya matope yaliyotokea Disemba 3, 2023 Kates Wilaya ya Hanang. mkoani Manyara.

................................................................

Na Mwandishi Wetu, Hanang'

 

TAASISI ya Asia Halamga Foundation chini ya Mhe Asia Halamga Mbunge wa vijana Taifa  leo tar 21.12.2023 imekabidhi majiko ya gesi 50  kwa lengo kusaiidia waathirika wa maporomoko ya tope Wilaya ya Hanang,

Mbunge huyo ambaye, hivi karibuni alikabidhi mahindi gunia 10 kwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang' Janeth Mayanja  ameendelea kutoa mkono wa pole pole kwa Wana Hanang kwa vitendo na kuahidi kuendelea na zoezi hilo hadi ndugu, jamaa, na marafiki walioathirika kurejea kwenye hali zao za kawaida  na kushiriki shughuli za maendeleo kama ilivyokuwa awali.

Akipokea maada huo Katibu Tawala wa wilaya hiyo,  Athuman Likeyekeye alisema wanamatumaini makubwa na mbunge huyo ambaye ameonesha  kwa vitendo na kutekeleza kwa nafasi yake kwa kuwakimbilia wananchi waliopatwa na athari za maporomoko ya tope wilayani Hanang'.

"Kitendo alichofanya Mbunge huyu ni cha kibinadamu na uzalendo mkubwa kwani ameunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha waathirika wa tukio hili wanapata mahitaji ya kibinadamu na ni ibada kubwa amefanya," alisema Likeyekeye.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad