TIA SINGIDA YATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA MAFURIKO HANANG' WAPONGEZWA KWA UZALENDO - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, 23 December 2023

TIA SINGIDA YATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA MAFURIKO HANANG' WAPONGEZWA KWA UZALENDO

Mhadhiri wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, Profesa David Msokwa, kwa niaba ya Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dkt, James Mrema, akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Hanang' Janeth Mayanja, msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na TIA kwa ajili ya  kusaidia waathirika wa mafuriko ya maporomoko ya matope yaliyotokea Katesh,  mkoani Manyara Disemba 3, 2023. Kushoto ni Mlezi wa wanafunzi wa taasisi hiyo, Asia Hancy.

......................................................

Na Dotto Mwaibale, Manyara

TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida imekabidhi vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh.333,750 kwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang'  kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko ya maporomoko ya matope yaliyotokea Katesh,  mkoani Manyara.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa TIA Kampasi ya Singida, Mhadhiri Dkt. David Msokwa alisema msaada huo umelenga kuunga mkono jitihada za Serikali kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko na maporomoko ya matope ya Mlima Hanang yaliyotokea Disemba 3, 2023 na kusababisha vifo na uharibifu wa mali ikiwemo mifugo na nyumba.

"Tumefika hapa leo kutoa mkono wa pole kufuatia janga la mafuriko lilitokea Disemba 3, 2023 tukiwa tumeongoza na Serikali ya Wanafunzi (TAISO) na Rais wao, Mlezi wa Wanafunzi, Asia Hancy pamoja na mwakilishi wa watumishi wa taasisi hiyo, Francis Majele kwani tukio ili nasi lilitugusa mno," alisema Msokwa.

Profesa Msokwa alisema vitu hivyo vimepatikana baada ya taasisi hiyo kufanya kazi za kijamii kwa kulipwa kama uoshaji wa vyombo vya moto, kushiriki michezo na kuchangia damu na kuwashirikisha wadau wengine ambao walichangia fedha na vitu vya aina tofautitofauti.

Alivitaja baadhi ya vitu hivyo kuwa ni viatu, madaftari, sabuni, chumvi, unga wa mahindi, mafuta ya kupikia, nguo, viberiti na maharage.

Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja akipokea vitu hivyo aliwashuru TIA kwa kuonesha uzalendo kwa kuiunga mkono Serikali kwa kuwasaidia waathirika hao.

"Kwa niaba ya Serikali nichukue nafasi hii kuwashukuru kwa kuleta vifaa hivi kama mnavyojua wakati tukio hili linatokea Rais alikuwa nje ya nchi kwenye ziara ya kikazi ambapo alilazimika kuiharisha na kurudi kwa ajili ya kuhakikisha waathirika wanapata mahitaji kama dawa na kurekebishwa miundombinu kwa haraka," alisema Mayanja.

Mayanja alisema kwamba jambo walilolifanya TIA ni la ibada na kuwa wanapaswa kuendelea kulifanya katika matukio mengine kama hayo yakitokea na kuwa wameonesha uzalendo mkubwa.

Mwakilishi wa wafanyakazi wa TIA Kampasi ya Singida, Francis Majele alisema wameguswa na tukio hilo na ndio maana wakaona ni vuzuri nao wafike kutoa msaada huo ikiwa ni kuiunga mkono Serikali.

Safari wa kuelekea Katesh wilayani Hanang' kutoa msaada huo ikifanyika. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad