CRDB TANGA YAJIPAMBANUA MIKOPO WAMACHINGA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Tuesday, 26 December 2023

CRDB TANGA YAJIPAMBANUA MIKOPO WAMACHINGA


Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba (katikati), akimkabidhi zawadi ya seti ya sofa Fatuma Omari baada ya kushinda shindano la matumizi ya Tembo Card lililoandaliwa na Benki ya CRDB, Kanda ya Kaskazini..

...................................................

Na Mashaka Kibaya, Tanga

BENKI ya CRDB imezindua utaratibu wa Mikopo kwa Wafanyabiashara wa Masoko 'Wamachinga' ambapo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amewataka watakaobahatika kukopa kutumia fedha hizo kwa dhumuni lililokusidiwa na kuzirejesha kwa wakati. 

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba jana katika Viwanja vya Tangamano Jiiini Tanga alikuwa Mgeni rasmi kwenye Shughuli hiyo ya Uzinduzi wa Mikopo kwa Wafanyabiashara wadogowadogo huku akiwanasihi kuzingatia matumizi sahihi ya rasilimali fedha watakazokopeshwa.

Kindamba alisema, alisema baada ya majadiliano na Benki ya CRDB kuhusu suala la Mikopo hiyo kwa Wafanyabiashara wadogo wadogo riba na dhamana vimekuwa rafiki kuwawezesha Wajasiriamali kukopa.

"Awali 'rate of interest' ilikuwa juu sana na mimi nilipata kuwa 'Bankers' kipindi cha nyuma nikasema Hapana.Wafanyabiashara wangewekwa kwenye mtihani,lakini sasa CRDB wamekaa na Viongozi wao sasa riba imeshuka na kuwa chini"alisema Kindamba. 

Kwa mujibu wa Kindamba Mkoa wa Tanga hivi sasa Mfanyabiashara akikopa Shilingi Milioni moja (Tsh 1 mil) baada ya mwaka mmoja atapaswa kulipa Shilingi 1,070,000 Mil.

Kutokana na mazingira hayo ya ukopaji kuwa rafiki kwa Wafanyabiashara wa Masoko, Mkuu wa Mkoa aliwataka watakaokopa kutumia fedha hizo kwa dhumuni lililokusidiwa.

Aidha Kindamba aliwasihi Wafanyabiashara kuendelea kutunza uaminifu kwa benki hiyo ya CRDB huku akiwaasa Wanaume kwa kuwasisitiza kutokutumia fedha hizo kwenda kuoa Wanawake wengine.

"Nitoe rai kwa Wanaume wenzangu,ukipata hizo pesa rudi nyumbani mkae meza moja na Mama mkaunde mipango kwa pamoja wacha kupanga peke yako,usipate mkopo ukaenda kuongeza jiko"alisema Kindamba. 

Kindamba aliendelea kusema kuwa kwa Mfanyabiashara mdogo atakayehitaji kukopa dhamana yao itakuwa Vizimba wanavyoendeshea shughuli zao ikiwa ni pamoja na kutambulika Uongozi wao wa Soko.

Kwa upande wa Mikopo ya Wasafirishaji wa Bodaboda na Bajaji, hao watatakiwa kulipa asilimia 20% ya malipo ya awali (down payment) huku riba yao ikiwa asilimia 15% na dhamana ya mkopo kuwa kadi ya chombo atakachopewa.

"Tunataka kurudisha Tanga iwe ya neema na hizi ni katika hatua tunazochukua kama Serikali, Wafanyabiashara walisema changamoto ni mtaji sasa mtaji unapatikana CRDB na dhamana imelegezwa"alisema.

James Kaji ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, amewashukuru Benki ya CRDB kwa kuanzisha utaratibu wa Mikopo kwa Wafanyabiashara wadogo wadogo hususani wale wa Bodaboda na Bajaji.

Alisema kundi hilo ni muhimu na linapaswa kusaidiwa huku akiwataka Bodaboda na Bajaji watakaokopa kuitumia vizuri mikopo yao na kuweza kurejesha.

Naye Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Cosmas Sadati alisema, wameamua kuishirikisha jamii ya Wafanyabiashara wadogo kuhusu suala la mikopo na mitaji huku wakiweka riba ndogo kuwawezesha kukopa.

"CRDB tumewaletea riba chini kabisa sasa Mfanyabiashara ashindwe mwenyewe,pia Bodaboda na Bajaji tumekuja kuwawezesha hawajitajiki kuwa na nyumba wala shamba kupata mkopo CRDB"alisema Sadati. 

Awali Meneja CRDB Mkoani Tanga, January Kirambata alisema,katika Shindano lao linaloendelea la kuhamaisha malipo ya Kidigitali na Tembo Card, Fatuma Omari Nundu ameibuka Mshindi na atazawadiwa Seti ya Sofa inayogharimu Kiasi cha Shilingi 8 milioni.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad