Sheikh Mkoa wa Singida, Issa Nasoro, akizungumza Disemba, 29, 2023 na Waislam wa Msikiti wa Ijumaa wa Tarafa na Kata ya Mtinko unaosimamiwa na Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) kufuatia taasisi moja ya kiisilam kudaiwa kufanya mchakato wa kusajili umiliki wa msikiti huo ikitaka kuuchukua wakati ni mali ya Bakwata.
(PICHA ZOTE NA SOLOMON PHILEMON)
.......................................
Na Dotto Mwaibale, Singida
SHEIKH Mkoa wa Singida, Issa Nasoro
amenusuru kuporwa kwa Msikiti wa Ijumaa wa Tarafa na Kata ya Mtinko
unaosimamiwa na Baraza Kuu la Waislam
Tanzania (BAKWATA) kufuatia taasisi moja ya kiisilam kudaiwa kufanya
mchakato wa kusajili umiliki wa msikiti huo ambao ni mali ya Bakwata.
Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na waumini wa dini ya kiislam Disemba
29, 2023 kwenye msikiti huo, Sheikh Nasoro ambaye alikuwa ameongozana na Mwanasheria Mkuu wa
Bakwata Taifa, Hassan Fatihu alisema kuna watu wamejitokeza kutengeneza taasisi
ndani ya taasisi.
“Tumekuja hapa baada ya kuwepo kadhia
kutokana na watu kujitokeza kwa ajili ya kupata usajili kupitia jengo la
msikiti huu tunao ujenga ambao ni mali ya Bakwata na jiwe lake la msingi
liliwekwa na Hayati Mufti Sheikh Mkuu, Hemed Bin Juma Bin Hemed Oktoba 28,
1990,’’ alisema Sheikh Nasoro.
Sheikh Nasoro alisema watu hao waliwarubuni
viongozi wa msikiti huo ambao walikuwa hawajui chochote na mara moja walianza mchakato wa kusajili
msikiti huo kupitia taasisi yao huku wakijua ni mali ya Bakwata.
Alisema baada ya kubaini jambo hilo waliwasiliana
na mamlaka mbalimbali na kufanikiwa kuzuia mchakato huo baada ya viongozi wa
msikiti huo kubaini kuwa walikuwa wamerubuniwa na watu hao.
Mwanasheria wa Bakwata, Hassan Fatihu
alisema msiki huo uliojengwa tangu mwaka 1945 ni mali ya Bakwata na si
vinginevyo ambapo aliwataka viongozi wa dini hiyo kujenga tabia ya kuuliza
jambo wasilolijua ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima kama huo ambao
umemsikitisha.
Muumini wa Msikiti huo, Juma Mene alisema
watu hao sio mara yao ya kwanza kuanzisha mgogoro huo kwani miaka ya nyuma
walifungua kesi iliyodumu zaidi ya miaka 20 ambayo iliipa ushindi Bakwata na
anashangaa kuona siku za hivi karibuni ukiibuka tena.
Mmoja wa Wajukuu wa waasisi wa msikiti huo
alisema katika Tarafa hiyo hakuna muumini yeyote wa dini ya kiisilam asiyejua
kama msikiti huo ni mali ya Bakwata hivyo hata kubali kuona kundi fulani
likitaka kuuchua labda wawaue kabla kufanya hivyo.









No comments:
Post a Comment